Breaking News

              Na Imelda Mtema

Mambo yanazidi kuwa mambo! Kwa mara nyingine Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ anatengeneza kichwa cha habari baada ya kumbonda mwandani wake, Wema Isaac Sepetu, ni Risasi Jumamosi pekee lililosheheni habari.

NI WIVU WA KIMAPENZI
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kazi yake ni kufuatilia mambo ya watu, Diamond anayetisha kwa sasa katika Bongo Fleva alifikia hatua ya kumtandika hadi akamharibu uso kisa kikielezwa ni wivu wa kimapenzi.
Ilidaiwa kuwa Diamond alikuta meseji ‘sms’ ya kimapenzi kwenye kilongalonga cha kiganjani cha Wema ndipo akapandwa na hasira akampa ‘kitu kinauma’.

ISHU ILIKUWA HIVI
“Ishu iko hivi; Diamond na Wema walikuwa wamepumzika mchana, ghafla jamaa alichukua simu ya Wema na kuanza kusoma sms, ndipo alipokutana na moja iliyoshiba mapenzi kutoka kwa mwanaume ikionesha kama wana uhusiano toka zamani,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Diamond hakutaka kuhoji zaidi, kilichofuata ni kipigo ambacho Wema hawezi kukisahau.”

WEMA KAMA MATUMLA
Chanzo kiliendelea kutambaa na mistari kuwa ilitokea purukushani kubwa ambapo Wema aligeuka bondia Mbwana Matumla kwa kupangua makonde ya Francis Miyeyusho kama alivyofanya wiki iliyopita pale Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

DIAMOND KAMA MIYEYUSHO
Ilidaiwa kuwa staa huyo wa filamu hakufua dafu kwani Diamond alipeleka konde moja matata kama lile la Miyeyusho kwa Matumla hivyo kumwachia michoro ya makofi usoni huku akimsababishia mrembo huyo kutosikia vizuri hadi sasa.
Baada ya kuinyaka habari hiyo ikiwa ya motomoto, ‘polisi’ wa Risasi Jumamosi
alisaga soli hadi kwenye saluni ya Joan iliyopo Kijitonyama, Dar ambapo Wema alikuwa akiweka kope.

WEMA AMWAGIWA UPUPU
Baada ya kumuona paparazi wetu, Wema alihoji kulikoni ambapo alimwagiwa ‘upupu’ wote na kupewa nafasi ya kufunguka juu ya ishu hiyo.
Kwanza alianza kwa kusita, lakini baadaye alifunguka: “Jamani mapenzi nyie acheni tu, ni kweli alinipa ‘mbata’, lakini hayo ni mambo ya kimapenzi tu kwa sababu mimi mwenyewe nasikia raha sana nikipigwa na mpenzi wangu.

‘AMENITHIBITISHIA ANANIPENDA’
“Asikwambie mtu, bila kunipiga atakuwa hana wivu na mimi, lakini alivyonipiga amethibitisha anavyonipenda.
”Napenda Diamond na nitampenda maisha, kama ni vipigo sijali acheni nitoke manundu.”

WE DIAMOND, NI KWELI UMEMPIGA WEMA?
Jitihada za kumpata Diamond ili kupata jibu kama kweli alimpiga hazikuzaa matunda.

No comments