Breaking News

2011


Na Mwandishi Wetu
Zimebaki siku tisa kabla ya kufunga ukurasa wa mwaka 2011 na matukio yake, yaliyojiri ni mengi, Amani linakuja na ripoti kamili ya kile kilichojiri kwenye tabaka la mastaa ndani ya Bongo a.k.a Jakayaland.
Wapo mastaa waliokumbwa na maradhi kisha kupata mateso makubwa, wapo waliopoteza maisha, wengine maji yalizidi unga, hivyo kulimana talaka, huku stori za wapenzi kusalitiana zikiwa zimetengeneza vichwa vingi vya habari.
Ripoti ya Amani ya mwaka 2011, inagusa pia matukio ya ajali nzito ambazo ziliibua mtikisiko nchi nzima pamoja na migogoro ya mastaa, ikiwemo kupigana.

UGONJWA
Hivi sasa, tabaka la mastaa lipo kwenye maombi, wakimuombea afua msanii Joseph Shamba ‘Vengu’ ambaye amelazwa Wadi ya Mwaisela,…
Na Mwandishi Wetu
Zimebaki siku tisa kabla ya kufunga ukurasa wa mwaka 2011 na matukio yake, yaliyojiri ni mengi, Amani linakuja na ripoti kamili ya kile kilichojiri kwenye tabaka la mastaa ndani ya Bongo a.k.a Jakayaland.
Wapo mastaa waliokumbwa na maradhi kisha kupata mateso makubwa, wapo waliopoteza maisha, wengine maji yalizidi unga, hivyo kulimana talaka, huku stori za wapenzi kusalitiana zikiwa zimetengeneza vichwa vingi vya habari.
Ripoti ya Amani ya mwaka 2011, inagusa pia matukio ya ajali nzito ambazo ziliibua mtikisiko nchi nzima pamoja na migogoro ya mastaa, ikiwemo kupigana.

UGONJWA
Hivi sasa, tabaka la mastaa lipo kwenye maombi, wakimuombea afua msanii Joseph Shamba ‘Vengu’ ambaye amelazwa Wadi ya Mwaisela, Hospitali ya Taifa, Muhimbili.
Mbali na Vengu, msanii mwingine anayesumbuliwa na maradhi ni Juma Kilowoko ‘Sajuki’, ingawa afya yake imeanza kuimarika.
VENGU
Alipoanza kuugua, ilionekana ni ugonjwa mdogo, lakini baadaye hali ilikuwa tofauti.
Alilazwa wadi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kwa zaidi ya miezi mwili kabla ya kuhamishiwa Mwaisela.
Kwa mujibu wa watu wa karibu, ripoti za madaktari zinaonesha kuwa afya ya Vengu inaimarika kwa kasi, lakini machoni uimarikaji huo, unaenda taratibu mno.
Habari zilisema kuwa Vengu anakabiliwa na matatizo ya mfumo wa damu kichwani, maradhi ambayo imeelezwa yanaweza kutibiwa hapa hapa nchini.

SAJUKI
Mwaka ulianza vizuri kwa upande wake, lakini ghafla afya yake ilianza kudhoofika baada ya kumaliza nusu ya kwanza ya mwaka 2011.
Habari zilieleza kuwa ingawa sasa Sajuki anaweza kutembea, tofauti na mwanzo alipokuwa wa kushinda ndani amelala lakini bado mwili wake ni udhaifu.

VIFO
Mwaka 2011, ulishuhudiwa kwa mastaa mbalimbali wakitangulia mbele ya haki.
Mwana-Bongo Fleva, aliyebuni mtindo wa ‘kurap’ kwa kutumia lafudhi ya Kimasai, Abel Loshilaa Motika ‘Mr. Ebbo’, alifariki dunia hivi karibuni katika kipindi ambacho hakijazidi hata mwezi mmoja.
Ebbo, alifariki duania kwa ugonjwa wa kukaukiwa damu mwilini.
Mbali na Mr. Ebbo, mwanzoni mwa mwaka huu, taifa lilikumbwa na mshtuko wa aina yake, kufuatia vifo vya wanamuziki 13 vya wasanii, waliokuwa wanaunda Kundi la Five Stars Modern Taarab.
Ajali ilitokea ndani ya eneo la Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, takriban kilometa sita kutoka lango kuu la kuingilia kwenye mbuga hiyo ya wanyama kutoka upande wa Dodoma.
Chanzo cha ajali hiyo kilikuwa ni mwendo wa kasi wa gari aina ya Toyota Coaster namba T 351 BGE, walilokuwa wamepanda wanamuziki hao ambalo liligonga lori la mbao, lililokuwa limeharibika barabarani.
Mastaa wa Five Stars waliopoteza maisha ni Issa Ally ‘Kijoti’, Husna Mapande, Hamisa Omar, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Nassoro Madenge, mpiga solo, Sheba Juma, mpiga gitaa la besi Omar Hashim, mpiga kinanda, Tizzo, mbeba vyombo, Omar ‘Tall’ na mtumishi mwingine wa kundi hilo, Ngereza Hassan.
Aliyekuwa Kiongozi wa Kundi la Sanaa za Maigizo la Jakaya Theatre, Thomas Senzighe, alitangulia mbele ya haki mwaka huu kwenye ajali ya kuangukiwa na kontena, iliyotokea Kimara, Dar es Salaam.
Wengine waliofariki dunia mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali ni msanii wa zamani wa Kundi la Chemchemi Arts ‘Kidedea’, Dalila Peter ‘Tabia’, mwanamuziki Kasaloo Kyanga na Miss Mtwara 2011-2012, Rahma Swai.
Wengine ni aliyekuwa Mnajimu Maarufu Afrika, marehemu Sheikh Yahya Hussein, aliyekuwa ripota wa ITV/Radio One, Maulid Hamad Maulid na aliyekuwa Mkurugenzi wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo sasa ni TBC, David Wakati.
Mwaka 2011, ulishuhudiwa kwa vifo vya wanasoka maarufu waliotikisa miaka ya nyuma, Juma Mkambi na Dankan Butinini.
NDOA NA TALAKA
Wapo mastaa waliofunga ndoa na wengine walimwagana na kurudiana ndani ya mwaka huu.
NDOA
Waliofunga ndoa ni Jacqueline Patrick ambaye aliolewa na mtoto wa mwanasiasa maarufu Bongo, Abdallah Fundikira, Abdullatif.
Wengine ni Joyce Kiria, Nargis Mohamed, Skyner Ally ‘Skaina’, Hadija Shaibu ‘Dida’ na Mwisho Mwampamba ambaye alimuoa mshiriki mwenzake wa Big Brother Africa ‘All Stars’ 2011, Meryl Shikwambane.
TALAKA
Skaina ilikuwa ndoa si riziki, kwani muda mfupi tu baada ya kuolewa, alijikuta anarudi nyumbani baada ya kulimwa talaka na mumewe.
Hata hivyo, sababu ya kuachana haijafafanuliwa upande mmoja lakini Skaina alisema alidai talaka baada ya mumewe kumtelekeza bila kumpa huduma yoyote.
Mwingine aliyepokea talaka mwaka huu ni mtangazaji wa EATV, Joyce Kiria ambaye aliachana na aliyekuwa mumewe, Nelson Nkongo ‘DJ Nelly’.
UGOMVI
Mastaa mbalimbali waliingia katika ugomvi wa hapa na pale, huku wengine wakifikishana kwenye vyombo vya sheria.
Aunt Ezekiel alidaiwa kumpa kipigo msanii mwenzake Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’ kwenye Klabu ya TCC, Chang’ombe, Dar, chanzo kikidaiwa ni mapenzi.
Jacqueline Wolper na Zuwena Mohamed ‘Shilole’, walipeana ‘kisago’ kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam.
Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ alidaiwa kumtwanga chupa Wolper, ingawa ilimchuna ‘kiduchu’ kwenye Pub ya Shilole, Kinondoni.
Shilole, alimvamia msuka nywele maarufu Kinondoni, anayeitwa Bonita na kumpa kipigo kwa madai ya umbeya.
Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, alimpa kipigo Wema Sepetu, chanzo kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.
MAPENZI, USALITI
Hivi karibuni, Wema alimtuhumu mwenzi wake, Diamond kwenda kinyume kwa kutoka kimapenzi na Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo.
Kwa mwaka mzima, Wema alikuwa kwenye uhasama na Wolper, akimtuhumu kujiingiza kwenye mapenzi ya Diamond.
Wanandoa, Irene Uwoya na Hamad Ndikumana ‘Kataut’, waliachana kwa saa 33, chanzo kikidaiwa ni tuhuma za usaliti ndani ya ndoa.
Uwoya, alidai kutumiwa ‘SMS’ zinazoeleza kuwa Kataut ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine ndani ya Bongo.
Kwa upande mwingine, Uwoya alimchana Wolper kuwa anamchafua kwa madai kwamba anamtangaza kutoka kimapenzi na boyfriend wake ambaye hakumtaja.

No comments