Breaking News

BEEF: DRAKE & COMMON ???!!!

weekend iliyopita stori kuwahusu marapa Common na Drake ilihusu DRAKE kuperfom kwenye consert ya radio 106fm ambapo kabla ya kushuka kwenye stage, alitamka kwamba “SITAACHA KUFANYA MUZIKI kwa mashabiki wangu,  I don’t give a f*ck, kama unakitu kuhusu mimi, nifate niambie na sio kwenda kuongea kwengine, sio kwa sababu naimba unichukulie poa, MIMI SIO MJINGA
inaaminika hayo maneno ameyatoa maalum kwa rapper COMMON ambae ana track mpya sasa hivi inaitwa SWEET ambayo amewachana marapa wanaoimba, ambapo ametumia lugha nzito na neno la tusi maarufu kwa wamarekani kuwatukana marapa wanaoimba.
leo katika interview moja ya radio huko CHICAGO, Common amesema kwa sababu DRAKE ameanza kutoa maneno kwa kuona kwamba hiyo track ina muhusu basi AKAE HUMO.
Common amesema aliwalenga wengi kwenye hiyo track, sasa kama mtu anajihisi amesemwa basi ndio yeye, na kuongeza kwamba wakati JAY Z alipotoa DOA, T PAIN alijishtukia wakati hiyo track ilitolewa kwa ajili ya wengi wanaotumia AUTO TUNE, so kama umejistukia ndo inakuhusu.

No comments