Breaking News

BONGO 50 PROJECT RELEASE ROMA FEAT JAY MOE
Yalaiti ambayo imeimbwa na msanii MwanaFa akiwa ameshirikiana na Linnah inapatikana kwenye Albam ya Bongo50 ambayo iko tayari inasubiri muda na siku tayari kuwa kwenye soko la muziki wa Tanzania, halikadhalika wimbo Zamani ambao umehuishwa na msanii Q chief akiwa amewashirikisha Barnaba na Linnah pia unapatikana ndani ya albam hiyo.


Na safari hii muendelezo wa ngoma hizi ambazo zimerudiwa  kwa malengo ya kuzilinda ili zisipotee kwenye medani ya muziki nchini, tunakutana na Mr Famous a.k.a Jay Moe a.k.a Superman a.k.a Moe Technins a.k.a Mohammed Mchopanga akiwa ameshirikiana na Roma Mkatoliki kwenye wimbo uliojizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki “Mvua na Jua” ukiwa umeandaliwa na kurekodiwa chini ya Production ya Bongo Records na P Funk Majani.


Hapo awali wimbo huu ulirekodiwa na Jay Moe mwenyewe japo kwenye Chorus alisikika Solo Thang kwenye sauti za ziada za kiitikio, na ulipatika kwenye Albam ya kwanza ya msanii huyo iliyokwenda kwa jina ULIMWENGU NDIO MAMA ambayo imeandaliwa kwa kurekodiwa ndani ya studio za Bongo Records mnamo mwaka 2002.


Song: Mvua na Jua

Artist: Jay Moe Feat Roma

Studio: Bongo Records

Producer: P Funk Majani.

No comments