Breaking News

DJ CHOKA AFUNGUKA KUHUSIANA NA SHOW ZA BONGO

HAWA NDIO BAADHI YA WASANII WALIOFANYA SHOW NYINGI KWA KIPINDI HIKI CHOTE CHA MWAKA 2011.

Ally Kiba ni msanii aliyefanya vizuri sana kwa mwaka huu 2011 kwa kutoa wimbo wake uliobeba jina la Dushedede. Wimbo huu umempa show kibao za ndani na nje ya nchi na kujikuta anafunga mwana vizuri na kuweka kumbukumbu kwa kufanya show nyingi na kuendelea kuongeza idadi ya mashabiki kote duniani.

Dully Sykes aka Brazamen aka Mr. Misifa, huyu bwana kwa mwaka huu ametoa wimbo uliobeba jina la Bongo Fleva nakupa show nyingi hapa bongo na nje ya mipaka ya bongo. Dully ni msanii ambaye kwa mwaka huu amepiga show nyingi hadi kufikia kuwa kwenye tangazo ya kampuni moja ya simu hapa nchini.

 Linah msanii bora wa kike kwa mwaka huu aliyefanya vizuri kwa kuchukua tuzo mbili za Kili Music Award, moja ikiwa kama Mwimbaji bora wa Kike na ya pili ni kama msanii bora anayechipukia. Pia kwa mwana huu Linah ameweza kwenda New York kwenye tuzo za mama Laura Bush na Atlanta  kwenye mkutano wa Ushers New Look Foundation. Linah kwa mwaka huu amepiga show nyingi sana hapa nchini kuandia Dar mpaka mikoni kwenye matamasha makubwa yanayoandaliwa.

AY ni msanii ambaye kila siku hufungua mipaka kwa wasanii wa kitanzania edha kwa kufanya show au kitu fulani. Kwa mwaka huu AY ameweza kunyakuwa tuzo kadhani kutoka Kenya na Uganda na pia kwa mwaka huu ameweza kufanya video na wasanii wawili wakimarekani Lamya & Romeo kwenye wimbo uliopewa jina la Speak Wit Ya Body. Pia kwa mwaka huu ameweza kuvuka mipaka kwa kupiga show Kenya, Rwanda, India, n.k

Bob Junior aka Rais wa Masharobaro mbali na kuwa Producer mzuri lakini kwa mwaka huu ameweza kufanya vizuri kwa kutoa nyimbo nzuri na kufanya show nyingi kwenye baadhi ya mikoa hapa nchini na mwishoni wa mwaka huu atafunga mwaka kwa kufanya show yake UK. 

Godzilla aka King Zilla msanii wa hip hop anayewakilisha vizuri pande zake za Salasala Mbezi Beach, Zilla kwa mwaka huyu ni moja ya wasanii waliofanya show nyingi sana hapa bongo. Ni mmoja ya wasanii ambao lazima atatajwa kwa kila show ambazo zitaandaliwa kokote.

Mwana FA aka Binamu msanii wakipekee ambaye akitoa wimbo hewani unakuwa msemo mitaani, yeye kwa mwaka huu ameweza kufanya show nyingi kwa hapa Bongo na pia akavuka boda na kwenda South Africa na India kupeperusha mziki wake. Kwa sasa Mwana FA anatamba na wimbo pamoja na video yake ya Yalaiti akiwa amemshirikisha Linah

Izzo Bizness  msanii aliyepiga show nyingi hapa bongo huku akiwa anatamba na kibao chake kilichopewa jina na Riz One. Wimbo huu ulimpa chati za juu kwa mwaka huu na kumpa show nyingi nchini na wimbo kuwa kwenye chat za juu kwenye radio mbalimbali nchini.

Belle 9 msanii anayeiwakilisha mkoa wa Morogoro toka atoke na wimbo wake wa Sumu ya Penzi hadi leo bado jamaa amesimama vile vile kwa kupata show nyingi nakufanya Collabo nyingi. Pia wimbo wake Nilipe Nisepe huu ulimnyanyua sana kwa mwaka huu nakumfanya kuvuka boda na kwenda kufanya show South Africa. 

Dogo Janja msanii kutoka TIP TOP Connection kiumri ni mdogo sana katika ulimwengu huu wa muziki wa Bongo Fleva, yeye kwa mwaka huu ameweza kufanya vizuri kwa kufanya show nyingi kwa muda mfupi ambao alikuwa yupo likizo shule inapokuuwa imefungwa

Mr. Blue msanii mwenye mapozi yakipekee anayetesa na wimbo wake wa Tilalila ambao kwa mwaka huu umempa show nyingi sana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Ingawa mwaka huu anaumaliza vibaya kwa kuondokewa na Mama yake kipenzi, pole sana ndugu yangu kaza moyo haya yote ni mapenzi ya mungu na sisi tupo kwenye safari hiyo. 

 20 Percent msanii mwenye sauti yakipekee kabisa ambaye kwa mwaka aliweza kuujulisha uma kuwa yeye mkali pale alipochukua tuzo 5 kwa wakati mmoja, 20% baada ya tuzo na kabla ya tuzo alikuwa anafanya show nyingi sana huko mikoani kuliko msanii yoyote bongo, baada ya tuzo aliendelea na kupiga show na kuna siku nakumbuka nilimuuliza kaka mbona mjini huonekani akanijibu choka nina mtoto bado mdogo anahitaji malezi mazuri ya baba.

Barnaba msanii kutoka THT kwa mwaka huu ukizungumzia wasanii waliofanya show za kutosha huwezi kumsahau na huyu. Yeye pia kwa mwaka huu ameweza kwenda New York kwenye tuzo za mama Laura Bush na Atlanta kwenye mkutano wa Ushers New Look Foundation

CPWAA msanii huyu ukizungumzia wasanii wanaofanya vizuri na ambao hutoa nyimbo ikiambatana na video yake huyu huwezi kumsahau kabisa. CP kwa mwaka huu amefanya show kupitia wimbo wake mmoja tu wa Action ambayo imemfanya mpaka kupata tuzo mbili za Kili Music Award na kupata show kama India, Malaysia na South Africa.

 Chege & Temba wasanii kutoka TMK Wanaume Family kwa mwaka huu wameongoza kwa kutoa ngoma kali na video kali na kwakupiga show nyingi hadi kuvuka boda kupeleka mikono juu UK

Diamond Platinum msanii mwenye makeke na mkiki mingi kwa mwaka huu jamaa ameweza kupata show nyingi sana na kuchukuwa tuzo kutoka Mombasa na kujikuta anapandisha dau la show tofauti na ile ya mwaka jana hahaaa. Sitaki kumwelea sana maana mengine nitaweka chumvi wakati mnayasoma kila siku kwenye magazeti.

 Joh Makini Mwamba wa kaskazini ni msanii wa hip hop anayeiwakilisha vizuri hapa bongo, kwa mwaka huu amepiga show nyingi sana na yeye pia kwa mwaka huu ameweza kuchukuwa tuzo ya Kili Music Award. Joh kwasasa anatamba na video yake mpya ya Bye Bye akiwa amemshirikisha G-Nako.

Prof Jay ni msanii ambaye mwaka huu ameongoza kwa kuchana mawingi kwa sana kwa safari za nje ya Tanzania. Mwaka huu ameweza kupiga show nyingi sana na kuweka kumbukumbu zake vizuri. Kwa mwaka huu Jay ameweza kufanikisha lile lengo lake namba moja kwa kuamia kwenye nyumba yake ambayo alikuwa akiijenga kwa mda mrefu sana toka akifanya kazi Tanga. Mbali na hiyo huyu akiwa anatamba na video yake Kama Ipo mwaka huu anaufunga mwaka na wimbo wake mpya unaoitwa Kamiligado huku akiwa kwenye hatua za mwisho kurekodi video ya mwimbo huo na kampuni ya Visual Lab mwishoni mwa mwaka huu .

Roma Mkatoliki msanii kutoka mkoani Tanga, huyu kwa mwaka huu ameweza kufanya vizuri kwenye kila show alizokuwa akizifanya kwenye mikoa mbali mbali na hata hapa Dar. Kwa mwaka huu na yeye ameingia kwenye orodha ya wasanii wa bongo fleva waliofanya show nyingi kwa mwaka huu 2011

NAOMBA NIELEWEKE HIZI NI TAKWIMU ZANGU NILIZOZIFANYA NA KAMA NIMEKOSEA NASTAHILI KUSAHIHISHWA.

No comments