Breaking News

Fally Ipupa adatishwa na mademu DarNa Musa Mateja
MWANAMUZIKI kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ipupa Nsimba a.k.a Fally Ipupa anayepiga mzigo na kuishi nchini Marekani, hivi karibuni alidatishwa na mademu wa Kibongo na kuamua kuita mmoja baada mwingine kisha kucheza nao stejini, Ijumaa Wikienda linakushushia.
‘Balozi’ wetu alimshuhudia Fally akipagawa na ‘totoz’ za Kibantu Desemba 2, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam katika Tamasha la Usiku wa Kiafrika lililoandaliwa na Club E.
Akiwa stejini huku akishangiliwa na umati, uzalendo ulimshinda Fally na kujikuta akitangaza kuwa amedata na dada zetu kwa namna wanavyojua kukata mauno, uzuri na mvuto walionao.
Fally ambaye anakijua zaidi Kifaransa kuliko Kiingereza, alimkaribisha Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ stejini na kugonga shoo kali huku Dully Sykes akipanda kumpiga tafu mkali huyo wa Dushelele.
Wengine waliowasha moto katika onesho hilo ni THT ikiongozwa na Grace Matata na wasanii kibao wa sarakasi na mazingaombwe ambao walifanya vizuri na kukonga nyoyo za mashabiki waliofurika ukumbini hapo.

No comments