Breaking News

......ARAAAA, 'CHOCHEENI KUNI'...........

 MSANII wa muziki wa mashairi nchini Mrisho Mpoto, maarufu ‘Mjomba’, amesema kuwa anatarajia kutoa kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Chocheeni Kuni’, wimbo ambao unalenga kutoa ujumbe mzito kwa jamii na Serikali kwa ujumla.

baadhi ya maneno yaliyopo ndani ya wimbo huo yanasema “Chocheeni kuni zilizoloa maji yapate moto ugali usongwe, Wakiwauliza waambieni na huu ni utani kama wakwenu,” hayo ni maneno ambayo yanapatikana katika shairi hilo.

Msanii huyo ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na aina yake ya uimbaji alisema kuwa ametoa kazi hiyo lakini anaamini wananchi watajua nini maana yake kwani utakuwa na lengo la kukosoa yote yaliyo mabaya.

“Shairi langu ni gumu sana lakini nirahisi endapo wasikilizaji wataweza kulisikiliza kwa umakini, pia najua wachambuzi wa sanaa ambao ni waandishi wataweza kujua nini nachokizungumza,” alisema.

Hata hivyo Mpoto aliwaomba Watanzania kuisubiri kazi hiyo kwani inavitu ambavyo vinaweza kuleta hamasa kwa Serikali katika kufanya kazi ambazo siku zote wamekuwa wakiahidi na kushindwa kuzitekeleza.

No comments