Breaking News

THE DREAM: single ya UMRELLA imenipa MAMILIONI

The DREAM akiwa na mke wake wa zamani, Christina Milian.
Mwandishi wa single kadhaa zilizowah kuiteka dunia kwenye ustaarabu wa muziki, mume wa zamani wa mwigizaji/mwimbaji Christina Millian, THE DREAM amekiri hadharani kwamba alipata dola za kimarekani milioni 15 baada ya kuiandika single ya UMBRELLA  kwa RIHANNA, ambayo ilipata mafanikio makubwa sana siku chache baada ya kutoka.
 
Hiyo ndio stori ya the dream baba wa watoto wanne, akiwemo mmoja aliepata na Christina, Japokua umri umesogea kidogo, the dream mwenye umri wa miaka 34, amesema bado hajaridhika na idadi ya watoto wanne alionao, ataendelea kuongeza wengine.
 
kazi yake ya uandishi wa nyimbo, ni moja kati ya vyanzo vyake vikuuu vya mapato, kama hufaham yeye ndio aliandika single yaBABY, ya Justine Bieber na Ludacris, ambayo iliuza mamilioni ya kopi na kusababisha list ndefu ya shows, ambapo anasema wakati alipoitwa na lebo ya DEF JAM kwa ajili ya kuiandika hiyo track, alikua NEW YORK, akawaambia maboss wa def jam kwamba wamlipie hoteli New York akae aandike hiyo single, lakini hao maboss wakachomoa.
Basi na the dream akasema, na mimi siwezi kuifanya hiyo kazi kama hamuwezi kufata masharti yangu, sasa baadae baada ya maboss hao kufikiria sana, ikabidi wakubali kumlipia hoteli, ndio akaiandika.

No comments