Breaking News

KINACHOMSUMBUA DULLY SYKES KWA SASA!

Dully Sykes mwenye shati jekundu, wakati wa kutengeneza video ya ACTION ya CP
mwimbaji DULLY SYKES amesema anakerwa na usumbufu wa mabinti anaoupata kila siku, wanaompigia wanasema wanampenda na wanataka mapenzi nae.
amesema “wamefanya mpaka hata facebok yenyewe siingii tena, najuta hata kwa nini nilijiunga fB, kila mtu yuko fB sasa hivi mpaka dada wa nyumbani ndio maana kila mtu anaweza kuandika chochote anachotaka kwa sababu anafaham jinsi ya kumpata Dully kirahisi, na huwa natukanwa pia wakati mwingine”
Dully ambae ni baba wa watoto wawili, ameweka wazi kwamba “sasa hivi nimeshakua mtu mzima na nahitaji kukaa na familia yangu, sijajiondoa fB ila siingii tena, na nitaifunga, kwa sababu mpaka wake za watu wananisumbua kutaka mapenzi na mimi”
kwa kumalizia Dully amesema “wanawake wanaomsumbua sana ni Watangazaji, mamiss, wasanii na wasichana wengine maarufu na nina msg zao wanataka mapenzi yangu, ndio maana siku hizi nimepunguza hata kwenda club manake huko ndio nakutana sana na wanawake ambao HAWANA ISHU, kazi kutafuta wanaume tu”

No comments