Breaking News

MARUFUKU vipindi vya BURUDANI katika TV & RADIO.


Mamlaka inayohusika kugawa vibali au leseni za utangazaji kwa mashirika ya habari nchini CHINA, imezuia vyombo vya habari vya nchi hiyo, yani RADIO & TV kuendelea kurusha vipindi vya burudani kwa asilimia 60.
 
Agizo hilo limepiga marufuku show za burudani kwenye radio na tv, kuanzia tarehe 1 january mwaka huu ambapo idadi ya showz za burudani, imeshuka kutoka 126 mpaka showz 38 tu kwa siku.
 
wakati wa jioni mara nyingi Town za China huwa hakuna watu, wameshawah majumbani kupumzika na kutazama showz kwenye TV, yani kama wakati ule ilivyokua kwa ZE COMEDY hapa bongo.
 
Amri hiyo imetolewa baada ya Rais wa nchi hiyo kuonya vikali kuhusu utamaduni na mila za kimagharibi kuingizwa China, yani vipindi vingi vya tv na radio vilikua na damu ya nchi za ulaya na America ambapo mpaka sasa
China ndio nchi iliyo na watu wengi wanaotazama TV duniani, idadi inayozidi bilioni 1 na milioni 300.

No comments