Breaking News

MAUZO YA T SHIRT YAMPA SHAVU IZZO BIZNESS!

mdogo wake Ally Kiba, Izzo B & Ally kiba
staa wa single ya “RIZI ONE” mkali kutoka GREEN CITY Izzo B ameondoka Dar leo kuelekea kwao kwa ajili ya shughuli moja tu ya kufungua duka lake la nguo.
akiongea exclusive na millardayo.com Izzo amesema duka hilo litakua Soweto Mbeya, na linatarajiwa kufunguliwa kesho au kesho kutwa akiwa ametumia mtaji wa milioni mbili na nusu.
B amesema ataanza na nguo za kiume kwanza alafu za warembo zitafata baadae.
amesema mtaji wa duka lake ulichangiwa kwa kiasi kidogo sana na pesa za show ya single ya RIZI ONE lakini pesa nyingi ya mtaji, ameipata kutoka kwenye mauzo ya T SHIRT za lebo yake ya ONGEA NA MSHUA, biashara ambayo amekiri kuuza sana na kuzikusanya pesa zake.

No comments