Breaking News

MSANIII DIAMOND APEWA SIKU 21.

                                                 Diamond na wacheza show wake, walipokua kwenye mahakama ya mwanzo Iringa january 9 mwaka huu
Wiki mbili baada ya hukumu ya kesi ya kumpiga mwandishi wa habari inayomuhusu mwimbaji DIAMOND PLATNUMS kusomwa, na mwimbaji huyo kuamriwa na mahakama ya Iringa kumlipa faini isiyozidi laki moja mwandishi huyo, leo ishu nyingine mpya imeibuka.
Ishu yenyewe ni kuhusu mwandishi huyo Francis Godwin  kutoridhika na maamuzi ya mahakama, na sasa kamtafuta mwanasheria wake ambae ameongea exclusive na millardayo.com.
mwanasheria huyo Paul Lekanoi amesema ” kutokana na taratibu zetu ni kwamba hatuwezi kumfungulia mtu mashtaka bila kumpa taarifa, hivyo tumemuandikia barua DIAMOND kumjulisha kwamba endapo hatomlipa Godwin hizo milioni 30ndani ya siku 21 zijazo, kama fidia ya kumdhalilisha na kumharibia mali zake, tutamfungulia MASHTAKA, hizi ni kanuni na taratibu ndani ya sheria namba 33 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
mdhamini wa DIAMOND akiwa na mwandishi Francis Godwin mwenye kesi na DIAMOND
mwandishi Francis Godwin amesema “DIAMOND alifanya dharau kwa kuomba radhi wasikilizaji, watanzania na mashabiki wake lakini hakuniomba mimi msamaha, hilo ndio kosa angekua ameniomba msamaha tusingekua tumefika huku, hakuna mtu ambae anapenda kudhalilishwa”
mpaka sasa bado DIAMOND hajazungumza chochote kuhusu hili lakini akipatikana, utakua wa kwanza kufaham kupitia

No comments