Breaking News

Promota atekwa baada ya NAS kutotokea kwenye show ANGOLA.

 
Nas.
Promota mmoja wa marekani pamoja na mtoto wake, wamesema walitekwa na watu wasio julikana baada ya rapa NAS kushindwa kutokea kwenye consert waliyokua wameiandaa usiku wa kuamkia mwaka mpya Angola, Africa.
 
TMZ wameamplfy kwamba Alloso, ambae ni boss wa AllGood Entertainment, amesema walitekwa na watu waliokua na bunduki, watu ambao ni waajiriwa wa promota mmoja wa angola, Henrique Miguel, ambae alilipa hela nyingi pia kushiriki kuandaa hiyo show.
 
Mji mkuu wa Angola.
Promota wa kwanza, mmarekani Alloso amesema alilipa jumla ya dola za kimarekani laki tatu na elf 15 kwa Nas na msanii mwingine ambae ndio alitakiwa kuianzisha show, Jemiah Jai, ambapo wote walitakiwa kupiga showz mbili, lakini hawakuonekana hata Angola kwenyewe.

Sababu za promota huyo mmarekani kutekwa, ilikua hofu ya promota wa angola baada ya kuona mshkaj angeweza kukimbia bila ishu kumalizwa, ambapo promota huyo mmarekani na mtoto wake, walishikiliwa tena na mamlaka husika kwa saa saba na kuachiwa baadae, na wote bado wapo Angola, wanasubiri mpaka pesa walizolipwa Nas na Jemiah zirudishwe huku sababu za wasanii hao kutotokea kwenye show hazijajulikana mpaka sasa.

No comments