Breaking News

Sharo MILIONEA apata AJALI

Shar
Sharo Milionea
Msanii/Muigizaji/Mchekeshaji SHARO MILIONEA amepata ajali mbaya ya bus leo saa mbili na nusu Asubuh Mikese, Morogoro.
bus hilo la TAQWA likitokea BURUNDI kuja DAR ES SALAAM, limepinduka mara kadhaa wakati likilikwepa lori lililokua linajaribu kulipita lori jingine bila, yani lilikua linaOVERTAKE bila kujua kulikua na bus linakuja.
Sharo MILIONEA alikua amekaa kwenye siti ya mbele kabisa kwa hiyo aliiona ajali yote, japo anasema hana uhakika kama kuna yoyote amepoteza maisha, abiria wengi wameumia vichwani, miguuni na mikononi, majeraha ambayo wameyapata kutokana na vioo kupasuka na misuguano mingine wakati gari linapinduka.
baada ya ajali, imebidi abiria wengine waishie Morogoro kwa ajili ya kupata matibabu, lakini SHARO MILIONEA na wengine, wameendelea na safari na sasa wako njiani wanakuja DAR ES SALAAM, ambapo abiria wengi wamepoteza mizigo, na Sharo kapoteza simu tu.
kwa sasa Sharo anaendelea vizuri japo sio sana kwa sababu anasikia maumivu mwilini, na akifika DAR atakwenda Hospitali kuchek.

No comments