Breaking News

ALICHOSEMA OMMY DIMPOZ KUHUSU HOFU YA KUTOA SINGLE NYINGINE!

                                        Ommy Dimpoz akiwa kwa stage..
Wanafamilia wa kigoma,  kwenye nafasi hii niko na ndugu kutoka huko huko, staa wa single ya Nai Nai, Ommy Dimpoz ambae ameamua kuuweka ukweli live sasa hivi, baada ya stori kuanza kupita kwenye midomo ya wengi kwamba mshkaji amechelewa kutoa track mpya kwa sababu anajifikiria mara mbilimbili na kusita kutokana na ukali wa single iliyotangulia ya Nai Nai.
Ommy amesema “sio kweli kwa sababu tayari Nai nai yenyewe ilikua na mwaka mzima imekaa tuu ndani kabla ya kuamua kuiachia na wala sikufiria kama ingekua ya kwanza kuitoa kwa sababu kuna nyimbo nyingine nyingi zilikuepo ndani tu nimeziweka”
Ommy Dimpoz ambae kabla ya kuwa solo alikua kwenye band ya TOP ya T.I.D ameamplfy zaidi kwamba “nina akiba ya nyimbo nyingine saba ambazo ziko tayari, hata VITUO VYA RADIO MBALI MBALI bado Nai Nai ni namba 1 kwenye top 20 bado inabamba ndio maana nataka kuipa time izidi kuhema, sitaki kuharakisha kutoa nyimbo nyingine japo nipo kwenye process za kufikiria kuachia singleya pili”

No comments