Breaking News

BOBBY BROWN APIGA SHOW MISSISSIPPI, AMUENZI WHITNEY HOUSTON

Pamoja na ndoa yao kukoma mwaka 2007 Bobby Brown na Whitney wanakumbukumbu nyingi za pamoja. Taarifa za kifo cha Whitney Houston zimemshitua sana Bobby Brown na watu wake wa karibu wanadai mchizi amekuwa na huzuni sana.

Hata hivyo wanamuziki wenzake wa kundi la New Edition wako karibu naye kumfariji kutokana na msiba huo. Hali hii imesababisha Bobby Brown kukosa wombo wa kwanza wa performance yao. Hata hivyo alimua kupanda jukwaa na kuendelea na performance kwenye concert ya Mississippi usiku wa kuamkia leo. Kitu cha kwanza kufanya jukwaani ni kusema "I Love You Whitney" ikiwa ni kumuenzi mtalaka..

Hata hivyo baadhi ya wapenzi wa muziki wa Whitney wanamlaumu Bobby Brown kwa kuwa chanzo cha kifo cha mwanadafada huyo wakidai yeye ndiye alimfanya ajiingize kwenye madawa ya kulevya. Ingawa ripoti ya kifo haijatoka wadau wanahusianisha kifo cha Whitney na madawa ya kulevya zaidi kuliko sababu nyingine.

Hata hivyo watu waliosoma high school na Whitney wanadai kwamba Whitney alikuwa cocaine addict toka alipokuwa shule na kwamba kumtupia lawama Bobby Brown ni makosa makubwa. Rafiki wa zamani wa Whitney, Jodie anaweka wazi kwamba kama kifo cha rafiki yake kimesababishwa na madawa ya kulevya basi Bobby Brown hapaswi kulaumiwa kutokana na ukweli kwamba Whitney alikuwa akitumia kilevi hicho toka wakati yupo high school kipindi ambacho hata alikuwa hafahamiani na Bobby. Hivi karibuni mtandao wa TMZ uliwahi kutoa taarifa ya rehabilitation ya Bobbi Kristina mtoto wa Whitney na Bobby Brown. Binti yao huyu ambaye baada ya ndoa kuvunjika alikuwa akiishi na Whitney amekuwa akitumia madawa ya kulevya kwa kiwango kikubwa na watu wengi wanamuona Whitney kama sababu ya mtoto wake kuharibikiwa.

No comments