Breaking News

JAFFARAI ATANGAZA KUJITOA KTMA!

.

Baada ya staa wa biberon Dully sykes kusisitiza tena jana kwamba hataki kushirikishwa wala kuhusishwa kwa namna yoyote kwenye tuzo za kili, leo tena msanii mwingine amejitokeza na kuutaja uamuzi wake.
Jaffarai amesema “nimeamua kujitoa kwenye hizi tuzo kwa sababu chache kubwa, toka nimekua solo artist huu ni mwaka wa tisa sasa hivi, toka elfu 2003 ndio nilianza kushine na single ya NIKO BUSY, na unapo mzungumzia Jaffarai ni mmoja kati ya wasanii ambao wametengeneza hits nyingi sana hapa bongo”
ameamplfy zaidi kwamba “nimekua nikivumilia sana hizi tuzo kwa miaka mingi, nilikua najipa matumaini kwamba kama mwaka huu sipo mwaka kesho naamini nitakuepo, lakini haijatokea hivyo, SIJAWAH KUWEPO hata kwenye NOMINATION za KTMA hata siku moja, kilichonifanya nijitoe ni kwamba sijawahi kupewa heshima ya kuwa nominated hata mwaka mmoja”
J anachoongezea ni kwamba “naona kama mchango wangu hauthaminiwi na watu wa KTMA, kuna mapungufu mengi nayaona kila siku, sijatendewa haki kabisa”
alipoulizwa na millardayo.com kama ameshaandika barua kwa Baraza la sanaa Tanzania kutangaza rasmi kujitoa, J amejibu “siko tayari na wala sina muda, sina time ya kupoteza kufanya hivyo, ninachoomba next time wasinihusishe kwenye tuzo zao haijalishi nimetoa nyimbo kali au sio kali, sitaki”
hiyo ndio kauli ya Jaffarai ambae amesema track zake mbili, SIO KWELI na MCHARUKO zilipaswa kuwepo kwenye tuzo za mwaka huu, kwenye category ya Dance hall, alafu SIO KWELI ingeingia kwenye video bora.

No comments