Breaking News

.........MABADILIKO MAKUBWA YANAKUJA........MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo, Mr. Blue a.k.a untouchable byser, amesema kuwa anafikilia kubadilisha staili ya muziki anaofanya kwani anahitaji kujikita kwenye kurap.

Alisema anahitaji kurejesha staili yake ya zamani, ambayo ndiyo iliyomtoa kitu ambacho anaamini kuwa hata mashabiki wake wanakisubiri kwa hamu kubwa.

Alisema katika kuonesha staili yake ya kurap, kuna wimbo mpya ambao anaratajia kuutoa hivi karibuni ambao utamuonesha namna alivyobandilika.

“Sihitaji kuimba kwa sababu najua staili yangu ambayo awali ilinifanya niwe katika chati ni Rap, hivyo mashabiki wangu wataona utofauti wangu katika ngoma mpya ambayo itakuwa hewani siku kadhaa zijazo,” alisema.

No comments