Breaking News

MKONGWE MWINGINE ADONDOKA, DUNIA YA MUSIC MAJONZINI... R.I.P WHITNEY HOUSTON

Whitney Houston amekutwa amekufa katika hotel ambayo pre-party ya Grammy inategemewa kufanyika leo Feb 12. Whitney ambaye alifikia katika Beverly Hilton Hotel ambayo ndio party ya awali ya grammy inafanyika alikutwa na umauti baada ya kuachana na rafiki zake ambao alikuwa akipiga nao mitungi. Ingawa mpaka sasa haifahamiki chanzo cha kifo chake, mashuhuda wanadai Whitney na rafiki zake walikuwa wakinywa sana.


Ray J, boyfriend wa Whitney Houston, amethibitisha kifo cha mpenzi wake ingawa wakati anafariki dunia yeye hakuwa naye. Ni tukio liloleta majonzi makubwa hasa ukizingatia uwezo wa kimuziki aliokuwa nao Whitney.

Whitney Houston ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 48, ameshinda tuzo lukuki katika tasnia ya muziki. Houston ni mshindi wa tuzo mbili za Emmy Awards, tuzo sita za Grammy Awards, tuzo 30 za Billboard Music Awards, tuzo 22 za American Music Awards. Albam yake aliyoiita "Whitney" ilikuwa albam ya kwanza ya mwanamuziki wa kike kufika namba moja katika historia ya chart za Billboard. Hiki ndo kipindi ambacho Whitney alikuwa katika kiwango cha juu huku akiuza nakala mil 200 za albam zake duniani kote

Houston ana honorary doctorate ya Humanities toka chuo cha Grambling State kilichopo Louisiana. Whitney ameacha mtoto, Bobbi Kristina ambaye alimpata katika ndoa yake na Bobby Brown iliyodumu toka 1992-2007.

Mtandao wa TMZ unadai kwamba kifo cha Whitney Houston kiligundulika rasmi jana Feb 11 majira ya 3:55PM PST, na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi kutafuta chanzo cha kifo hicho ingawa taarifa za awali zinadai hakuna dalili zozote za mauaji au kujiua.

Ulimwengu wa muziki unaendelea kukumbukwa na vifo vya nguli wa muziki ikiwa ni miaka miwili tu toka mkongwe mwingine mfalme wa Pop duniani Michael Jackson kuiaga dunia katika kifo ambacho pia kiliacha maswali mengi kuliko majibu.

REST IN PEACE
WHITNEY HOUSTON (1963-2012)

No comments