Breaking News

NIMESHAWAAMBIA SITAKI MNICHAGUE KWENYE TUZO ZENU...ANG'AKA BROTHERMEN DULLY SYKESMkali wa Bongo Fleva amezitema tuzo za Kilimanjaro na kuwataka waandaji kumuondoa katika orodha.

"Sihitaji kuwepo kwenye tuzo zozote za Tanzania, sijawahi kufaidikia chochote kutoka kwenye tuzo hizo, kwa miaka 12 nipo kwenye muziki na nimepata mafanikio makubwa tu ambayo hayajachangiwa na tuzo zao" aling'aka Dully

Dully aliendelea "Hawajawahi kuona umuhimu wangu miaka ya nyuma walidhani labda nitafulia na kuishia njiani, kama wangejua thamani yangu wangeanza kunipa tuzo tangu kipidi kile cha single za Lady free, Julietha, Hi, Salome, Handsome na nyingine ndizo nilistahili kupewa tuzo kuliko hata wasanii wengine waliopewa ambao sasa hivi wamepotea kwenye ramani ya muziki"

Tuzo za Kilimanjaro zimezikilalamikiwa si tu na wasanii bali hata wadau wa muziki. Toka kuanzisha kwake Kilimanjaro Music Awards zinakabiriwa na changamoto ya kuwaridhisha wapenzi wa muziki ambao wengi wanaamini kuna mkono wa mtu wakati wa utoaji tuzo hizo..

Dully si msanii wa kwanza kujitoa kwenye tuzo hizo, kuna kipindi bendi ya muziki wa Dansi ya FM Academia waliwahi kufanya hivyo hivyo..

No comments