Breaking News

ROSE MUHANDO KATIKA LINE MOJA NA BEYONCE!!
hii ndio picha waliyoitoa SONY, picha ambayo wamemuweka pia Rose Muhando pamoja na wasanii wengine wanaofanya kazi na kampuni hiyo kama Beyonce, T Pain, Maria Carey, Sean Kingston, Alicia Keys, Pitbul.
Mkali wa Gospel Tanzania Rose Muhando ametangazwa kuwa msanii wa kwanza Afrika  kuchaguliwa kuingia mkataba na kampuni kubwa na maarufu duniani inayojihusisha na biashara ya muziki ya SONY (ukiacha wasanii wa Afrika Kusini)
kampuni za Sony na Rockstar 4000 iliyowahi kumpa Ally Kiba dili la kufanya kolabo na R.kelly ndio zimetangaza hii ishu leo Dar es salaam.
Mwakilishi wa Rockstar 4000 upande wa kipaji Afrika Seven Mosha amesema japo kwa sasa hawawezi kutaja kiwango cha pesa atakachopata Rose Muhando baada ya kupata hilo dili, mkataba wake ni wa miaka mitano.
Amesema baada ya movie zake kutengenezwa, vitabu vyake pamoja na vitega uchumi vingine ndio wataanza kutaja mapato yake.
Seven amesema katika mchujo walioufanya mpaka kumpata Rose Muhando, ulihusisha wasanii wengine nane wakubwa wa Tanzania, waimbaji wa Gospel na Bongo Fleva na pia walikua na idadi nyingine kubwa ya wasanii wa nchi nyingine za Afrika kama Nigeria ambapo mwisho wa mchezo, Rose Muhando akashika nafasi ya kwanza.
Katika mkataba huo, tayari Rose Muhando amerekodi album nzima Afrika kusini kazi ikiwa imesimamiwa na Sony ambapo amepata nafasi ya kufanya kolabo na wasanii wengine wakali wa gospel wa nchi hiyo ambao watatajwa soon.
katika sentensi nyingine, Seven amesema mkataba huo haumfungi Rose Muhando kurekodi nyimbo zake na studio yoyote Tanzania, japo mpango wa Sony sasa hivi ni kumpeleka juu zaidi kwenye mauzo ya kimuziki Afrika ambapo atatumia lugha hiyo hiyo ya kiswahili.

No comments