Breaking News


Habari zenu wadau! Nimeona nifanye kushare nanyi nyimbo za wasanii hawa wawili. Track ya kwanza ni ya dogo anaitwa Adam Kanyama (born 1995) rapper na mwandishi wa nyimbo ambaye amekulia huko Norsborg,Stockholm Sweden. Mama yake ni mswedish lakini baba yake ni Mtanzania. Dogo ameanza kuchana tangu akiwa na miaka 11 na alikuwa kwenye kundi liitwalo "The Basicz" akiwa na Jordan Peltier na Chris Kipa. Track ya pili Nisher ni ya ama Nic Davie ( 1989 ) Huyu ni producer, mwandishi wa nyimbo,mmiliki wa studio ya kurekodi muziki mjini Arusha na muongozaji wa video za muziki. Alianza muziki tangu mwaka 2000. Aliamua kwenda Marekani mwaka 2005 kusomea masuala muziki na Televisheni. Ana record lebo yake mwenyewe iitwayo NISHER ENTERTAINMENT yenye makazi yake Arusha. Naomba muda wenu kusikiliza vipaji hivyo na pia ukivutiwa navyo ni vema kuvitangaza sababu vinapeperusha bendera ya Tanzania. Kazi njema, Skywalker.

No comments