Breaking News

HILI NDIO BASI LILILOTEKETEA KWA MOTO MOROGORO JANA USIKU.

Basi la kampuni ya Muro Investment, T820BEY lillilokuwa likitokea Mwanza kuja Dar es Salaam limewaka moto na kuteketea kabisa maeneo ya Maseyu Mkoani Morogoro jana usiku May 8 2012 saa moja na robo na hakukua na madhara yoyote kwa abiria ispokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto.
Mmoja wa wahusika wa basi hilo alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme ambapo ilitokea hitilafu kwenye taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari lakini walipofika Maseyu likashika moto.
.
hapakuwa na askari wala magari ya zima moto yaliyoweza kuwahi kufika na kuzima moto huo.
Wakazi wa Maseyu na abiria wakiangalia lilivyokua likiteketea. (picha zote zimepigwa na Mroki wa mrokim.blogspot.com )

No comments