Breaking News

NEW TRACK : Ben Pol - Pete
Pete  ni wimbo wa kwanza wa Ben Pol tangu aachie albam yake iitwayo Maboma akiwa chini ya MLab. Kwa maana nyingine ni kuwa huu ndio wimbo mpya aliorekodi akiwa nje ya label ya MLAB. 

"Thank God it's been a great journey and I personally feel the singles of that album were great. I have now come with a new production team and heading for my second album. Share it and I hope you enjoy this record as much as I enjoyed recording it. Peace and much love," ameandika Ben kwenye maelezo yake.

Wimbo huu umendikwa na waandishi watatu akiwemo yeye mwenyewe Ben Pol, Fred Max na Lady Peace Winnie.. Producer ni Mona Gangsta wa Classic Sounds.

Mashairi

Verse 1;

Hadithi ya penzi langu umenikata nini mwisho
huthamini huoni pendo lako nalihitaji leo kesho
 nishawahi kukosa ,mwenzenu nilisumbuka
 mchana na usiku mimi, nishawahi kukosa
nasema niliteseka mchana na usiku mimi
nishawahi kukosa ,mwenzenu nilisumbuka
 mchana na usiku mimi, sitaki tena kosa
najua nitateseka
mwisho sitokuwa nawe tena naulizaa
Chorus;

Kama pete yangu, inakuchomaa kidoleni
ni kama pendo langu , linakuchoma moyonii ,
bora kuitoa aaah aah ,
pendo kulivua aaah ,
bora kuitoa ,
moyoni mwangu mi nisiteseke
bora kuitoa aaah aa ,
pendo kulivua aaah ,
bora kuitoa ,
moyoni mwangu mi nisiteseke
Verse 2;

sikujali wambea wanafki walosema
hatutadumu mimi nawe tutajaachana
wakiniona siko nawe si ndo watasema
hata nyumbani watajua tumefarakana
nikiwaza kwenda mbali ,moyoni nahofia
maana bado nakujali ,kwako nilishatua
nikiwaza kwenda mbali ,moyoni nahofia
maana bado nakujali ,kwako nilishatua
kila jema n'tendalo mie ,kwako limekuwa sio
nitakapo kujua ulipo ,wanijibu utakavyo
pete kidoleni mwako ,yanisuta mwenzio
ndo maana nikukosapo ,moyo wanienda mbio

No comments