DAKTARI AMEELEZA KILICHOMUUA KANUMBA. NI BAADA YA JOPO LA MADAKTARI
MUHIMBILI KUMFANYIA UCHUNGUZI MSANII nyota wa filamu nchini, Steven
Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo
linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu
zimeeleza. Taarifa hizo za ndani, zilizopatika
na
jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa
tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya
siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe
gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo
kwa zaidi ya saa mbili. “Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu
kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa
marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain
Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa
ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji
(cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo,
ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua
kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo
wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana
katika mwili wake. “Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa
upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na
rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa
kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.” “Mtu
aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na
hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla
hajafariki.” Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye
pia aliomba jina lake lisitajwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa
umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa
upumuaji. Alisema sehemu ya maini na majimaji ya machoni ya marehemu,
vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au
kitu kingine katika mwili huo.
posted byDullayo D-timing on facebook
No comments