HUU NDIO UTABIRI WA KANUMBA KUHUSU KIFO CHAKE.
Zakayo Magulu alie kwenye Camera.
Producer/Editor na Director
msaidizi wa Marehemu Steven Kanumba ambae amefanya nae kazi kwa miaka
saba mfululizo Zakayo Magulu, amesema Kanumba ni kama alijitabiria kifo
chake kwenye movie yake mpya ambayo haijatoka bado.
Zakayo ameamplfy “hiyo movie
inaitwa LOVE & POWER ambayo imekamilika kwa asilimia 60, ambapo
stori yake inahusu Kanumba kumsaidia mwanamke figo ambapo baadae
wakaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi kama mume na mke lakini baadae
Kanumba akagundua yule mwanamke ana mwanaume mwingine, sasa yule
mwanamke akakasirika akamsukuma Kanumba ambae alitonesha figo na
kupelekwa hospitali”
Marehemu Kanumba akiwa na Zakayo Magulu
Kwenye sentensi nyingine Magulu
amesema “kilichonishangaza sasa ni kwamba kwenye sinema, Daktari
aliemfanyia operesheni baada ya kupata hilo tatizo, ndio daktari huyo
huyo aliekuja kumuhudumia Kanumba alipoanguka juzi nyumbani kwake, alafu
kitu kingine kinachonifanya nishangae Muhimbili baada ya kufariki
Kanumba wasanii wameshafika pale, msanii ambae kwenye hiyo movie
alimuona Kanumba kwa mara ya mwisho akiwa amefariki dunia ndio msanii
huyohuyo aitwae Kupa ambae pale Muhimbili ndio amemuona Kanumba kwa mara
ya mwisho na kufunga droo ya maiti, hii ilikua inatabiri lakini sisi
hatukufahamu chochote wala Kanumba hakuwahi kuongea kwamba angefariki
karibuni japo kulikua kuna vitu alikua anahuzunika navyo ambavyo vilikua
vikimtesa moyoni”




No comments