TAARIFA KUTOKA KWA AFANDE SELE+++++++KUHUSU ISHU YA KUKAMATWA KWAKE YEYE NA 20%++
"""Ndugu zangu ambao ni mashabiki wangu!! Juzi wakati nimerejea
kutoka Tanga, majira ya jioni ndugu zangu Ballet Wallet(mtupori) , Adam
Lumbe na Twenty Percent (20%) walitoka na gari yangu, kwa bahati nzuri
au mbaya wakapita maeneo ya NMB hapa
Morogoro, wakapaki gari kwa haraka kwa kuwa Adam Lumbe alimuona kijana
ambae alimtapeli katika mauziano ya pikipiki, likatokea zogo!! Polisi
waliokuwa Lindo pale Bank wakaja kuizuia gari na pia wakawaweka chini ya
Ulinzi Ballet Wallet na Adam Lumbe, licha ya maelezo waliyowapa
hawakuwaelewa, 20% akataka kuchukua gari wakamkatalia, ikabidi akodi
pikipiki aje nyumbani kunifuata nikafuate gari, nimefika pale Bank
polisi wakakataa kunipa gari ili niende kituo kikubwa cha polisi
kuwawekea dhamana ndugu zangu kwa kuwa muda huo Ballet na Adam walikua
washapelekwa kituoni, kilichotokea baada ya hapo nilielezwa nisubiri
gari ya doria nipewe Eskoti mpaka polisi lakini baada ya kufika gari ya
doria wakiwa na wanamgambo wa manispaa walituvamia na kuanza kutupiga
marungu na kutujerehi, wananchi ambao ni kama ndugu zangu wanamorogoro
wakasogea eneo la tukio, Polisi wakafyatua risasi hewani
kuwasambaratisha tukapelekwa Polisi kituoni, pale hatukuchukuliwa
maelezo haraka, baadae tukatoa maelezo baada ya wale mabwana wadogo
askari kupata amri toka kwa wakubwa wao!! Jana tukafikishwa mahakamani
tukakosa dhamana, tukapelekwa ngome (jail) tukiwa kama mahabusu, leo kwa
bahati nzuri tumepata dhamana, na tumeweka wanasheria makini kusimamia
HAKI yetu. si kweli hata kidogo kuwa kwenye gari yangu kulikua na silaha
za kijadi kwa lengo la kumdhuru mtu, walikuta fimbo yangu ile ya Mfalme
wa rhyemes na kisu au kama panga ambao ni kitu cha kawaida kuwa nacho
kwenye gari, na si kweli hata kidogo kuwa Ballet alikua kavaa kic..p*
tu. Ndugu zangu wapendwa watanzania wenzangu,na mashabiki wetu kiukweli
hali za jela na selo zetu ni mbaya mazingira mabovu ndugu zetu
wanateseka. Nilitumia muda mchache niliokua kuwa kule kuwafariji na
kuwapa moyo ingawa nilienda kwa Matatizo, na muda huu nipo hapa Nyumbani
Misufini na Twenty Percent na Ballet pamoja na ndugu wengine!
Tumechinja Mbuzi kama Sadaka au dhabihu kwa Mungu na kuchoma, kuelekeza
moshi kwake kama ishara ya kumpenda na kushukuru kwa yote!! mwisho
tunaomba radhi kwa mashabiki wetu wote kwa usumbufu mulioupata. ASANTENI
KWA FARAJA ZENU KWANGU WAKATI WOTE ,Ni mimi SELEMANI ABDALLAH JUMA
MUTABHAZI MSINDI .. KING OF RHYEMEZ. (AFANDE SELE)"" + MWISHO WA
KUMNUKUU..



No comments