Breaking News

Naibu waziri alivyomfungia Roma leo na kumpa onyo Nay wa Mitego

Naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Juliana Shonza leo amefanya mkutano na waandishi wa habari uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu sanaa na kuzifungia nyimbo kadhaa za Bongofleva kwa madai ya kuharibu maadili. Naibu waziri Shonza pia leo ametangaza kumfungia miezi sita kutojihusisha na muziki, wala kufanya show msanii Roma Mkatoliki kwa madai ya kukaidi wito wa BASATA, kutokana na kuimba wimbo wa Kibamia unaodaiwa kuwa hauna maadili.

No comments