Breaking News

WEMA NA DIAMOND NGOMA DROO

Na Musa Mateja
http://globalpublishers.info/
Penzi linalomilikiwa na mastaa wawili Bongo, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ (21) na shugamami wake Wema Isaac Sepetu ‘limefumuliwa’, ikidaiwa eti, limekutanisha watu ambao wanalingana kwa idadi ya wapenzi ‘waliopita’ nao, Ripoti ya Risasi Jumamosi imekamilika, shuka nayo.
Gazeti hili limeelezwa na vyanzo vyake kuwa, kabla ya kukutana, kila mmoja alikwishatajwa kwenye dhambi ya uzinzi na wapenzi wanaofikia wanne hivyo ngoma kuwa droo.

WATANO WA WEMA NI HAWA
Kwa kinywa chake, Wema anakiri kutoka kimapenzi na wanaume kadhaa huku akiomba chondechonde: “Jamani TID (staa wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed) na Blu (Herry Samir, naye msanii wa Bongo Fleva) naomba muwatoe kabisa kwani hawakufaidi penzi langu.”
Kwa kauli hiyo, ukiwaondoa TID na Blu ambao nao aliwahi kudaiwa kutoka nao, listi inayobaki ambayo ilithibitishwa na Wema mwenyewe ni kama ifuatavyo;
KANUMBA
Steven Charles Kanumba, akitumia cheo chake cha uigizaji na udairekta katika tasnia ya filamu za Kibongo, mwaka 2008 alifanikiwa kumshawishi mlimbwende huyo kuingia kwenye uigizaji na baadaye wakazama katika ‘malavidavi’ kabla ya kumwagana kwa skendo huku Kanumba akimburuta Wema mahakamani kwa kuvunja kioo cha gari lake.
JUMBE
Mjasiriamali Jumbe Yusuf Jumbe alifanikiwa kuonja penzi la Wema mwaka 2009 na kama ilivyokuwa kwa Kanumba, naye alimwagana na mnyange huyo kwa kashfa na maneno ya shombo kedekede.
HARTMANN
Mara baada ya kuchomoka mikononi mwa Jumbe, mwaka huo huo wa 2009, Wema alidaiwa kuangukia kwa ‘the big boss’ wa Hartmann Production, Hartmann Othmun Mbilinyi lakini baadaye alijiweka pembeni kuepuka msongamano na safari ya mapenzi ikaendelea.
CHALZ BABA
Siku chache kabla ya kutimkia nchini Marekani mwaka 2010, Wema alitangaza kuolewa na mwanamuziki wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta, Charles Gabriel Mbwana ‘Chalz Baba’ baada ya kukolezwa na ‘malavu’. Akaondoka nchini, aliporejea, alikuwa amekwishabadili upepo na moyo wake ulishamdondokea mtu mwingine hivyo wakatengana kwa maneno ya hapa na pale.

DIAMOND
Wakati Diamond akiwa juu kimuziki mwaka 2010, ghafla zikavuja habari kuwa yeye na Wema huwa wanachati kwa muda mrefu kwenye Mtandao wa Facebook, baadaye wakasimama mbele ya kamera ya gazeti ndugu na hili, Risasi na kuanika mapenzi yao.


WATANO WA DIAMOND NI HAWA
Kabla ya kukutana na Wema, Diamond aliwahi kuripotiwa akidaiwa kupeana ‘kampani’ na warembo wafuatao;
REHEMA
Akiwa amepata jina kupitia Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian ‘Video Queen’, mwaka huo alikiri kuwa: “Jamani Diamond ni mtu wangu ‘so’ wasichana wa mjini kaeni mbali naye.” Alipoulizwa Diamond anayetamba na ngoma yake mpya ya Moyo Wangu, akacheka sana, akakata simu na penzi lao lilisambaratika 2010.
WOLPER
Mwaka huo huo, wakati kukiwa na ‘rumansi’ kuwa Diamond anapeana ‘tafu’ na staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Masawe Wolper, ghafla Rehema akafungua kinywa: “Wolper niachie Diamond wangu.” Baada ya kauli hiyo, Diamond na Wolper wakafyata mkia na hawakusikika tena.
PENDO
Mwaka jana, pia Diamond aliripotiwa akidaiwa ‘kutoka’ na staa wa Maisha Plus Season II, Upendo Mushi ‘Pendo’. Diamond alipotafutwa ili kupata mzani wa habari hiyo, akaruka futi mia na ukawa mwisho wa penzi lao.

NATASHA VS WEMA
Mwanzoni mwa mwaka huu, gazeti tumbo moja na hili, Amani lilitonywa kuwepo kwa mrembo aliyetajwa jina moja la Natasha ambaye alidaiwa ‘kumfia’ Diamond. Hata hivyo, wakati mawasiliano kati ya Diamond na Natasha yakiendelea, Wema ambaye ndiye alikuwa amejitwalia penzi la msanii huyo, akaenda mstari wa mbele na kuharibu kila kitu.
Wema na Diamond ni wapenzi ‘hoti’ kwa sasa ambao wameahidi kufunga ndoa ‘soon’.

No comments