Breaking News

.......NAFURAHI KUFANYA MUSIC NCHINI KENYA......


MSANII wa muziki wa kizazi kipya ambaye kwa sasa anafanya kazi hiyo nchini Kenya Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema kuwa anafurahia kuishi nchini humo kwani anafanya muziki kwa raha bila karaha kama bongo.

Akifanya mahojiano maalumu kwa njia ya mtandao wa kijamii wa facebook, Ray C, alidai kuwa tangu alipofika nchini humo amekuwa akifanya mambo yake kwa umakini mkubwa kuliko alipokuwa Tanzania.
Alisema kuwa hata hivyo kitu ambacho kinamsukuma endelea kuishi nchini humo ni kutokana na nafasi aliyonayo ya kuweza kujitangaza kimataifa kwani ni nchini ambayo wasanii wake wanafanya muziki unaendana na soko la kimataifa.

“Muziki wa Kenya huwezi kuufananisha na Tanzania hata wasanii wa huku wako juu sana na wanafanya kazi siyo kutupiana majungu kama baadhi ya wasanii wa Tanzania,” alisema.

Hata hivyo alipoulizwa ni lini atarudi nchini, alijibu “Dah sifikili kuja Tanzania kwa sasa kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya ambayo yanahitaji nitulie kweli ili huko ni nyumbani nitakuja tu,”.

No comments