HILI NALO NENO
Japokua
watu wengi walikua wanategemea kwamba kwenye interview ya kwanza
atakayoifanya Rihanna baada ya kusherehekea birthday yake na mpenzi wake
wa zamani Chris Brown, angemzungumzia Chris Brown au kutoa majibu
tofauti kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi, ishu imegeuka tofauti.
Baada
ya kualikwa kwenye show ya Jonathan Ross London Uingereza, Rihanna
aliwashangaza watu kuhusu jibu alilolitoa kuhusu msimamo wake wa
kimapenzi sasa hivi kwani wiki moja iliyopita baada ya Chris Brown
kutokea kwenye birthday party yake na wawili hao kuonekana wakikaa
kwenye mapozi ya mahaba, wakiwa wameshikana mikono, kukumbatiana mara
kwa mara pamoja na kisses kuhusika, wengi walisema kazi imekwisha…… yani
Chris Brown amerudiana na Rihanna, na walipotoa wimbo wao pamoja, ndio
hizo habari zikazidi kukolezwa kabisa.
Sasa
turudi kwenye show ya Jonathan Ross, kilichotokea ni kwamba Rihanna
mwenyewe kwa mdomo wake, amekubali kwamba bado yuko kwenye maisha ya
upweke, hana mpenzi kwa sasa, na anamiss kuwa kwenye mapenzi kwa sababu
ameyachoka maisha ya upweke.
RiRi
amesema ana hamu ya kumpata mtu ambae atamridhisha kimapenzi, hicho
ndio kitu pekee anachokubali kwamba ana kimis sana kwa sasa, anataka
aina ya mwanaume atakaempata awe ametulia na mcheshi.
Wengi
walidhani angekubali kwamba karudiana na chris brown, sijashangaa sana
imekuaje Jonathan hakumuuliza kuhusiana na stori za kurudiana na Chris
Brown, inawezekana kabla hawajaanza interview labda Rihanna aliomba hiyo
ishu isizungumziwe manake ingemuharibia zaidi watu wengi wangemshangaa
kurudiana na mwanaume ambae alimpiga na kesi yao ilikua kubwa.



No comments