WEMA SEPETU AJIBU BAADA YA KUFANYIWA FUJO NA MKE WA MTU!
hii
ni moja kati ya picha alizopiga wakati alipokua akifanya shopping huko
Dubai, shopping ambayo inadaiwa alipelekwa na huyo pedeshee!
Baada ya kuletewa fujo weekend
iliyopita na mwanamke anaedai muigizaji Wema Sepetu amemuibia mume, leo
mrembo huyo (Wema) ameamua kuzungumzia upande wake ambapo kama
haukuingia millardayo.com juzi march 5 kulikua na stori ya huyo mwanamke
kumfanyia fujo Wema baada ya kumkuta yeye na wasanii wenzake ndani ya
Pub ambayo inamilikiwa na mwanamke huyo.
Wema amesema “kwanza mimi
mwenyewe nilishtuka sana, nilikua natafuta location ya kucheza movie
yangu kwenye mgahawa, nikawa nimepaki nje kutoka na kurudi nikamkuta
mwanamke ndani ya gari jeupe limepaki pembeni yangu siijui wala huyo
mwanamke simjui nikamchukulia kama mmoja wa haters, akaanza kufanya fujo
wakati mimi huwa siwezi fujo, nikajitahidi kutoka eneo la tukio na
kupiga simu polisi na kuja kumchukua huyo mwanamke na kwenda polisi
Osterbay”
“Kiukweli sitembei na mwanaume
wake, sitembei na mume wa mtu……. alafu yule ni mwanamke mtu mzima sana
hawezi kugombana na mimi, mi mtoto mdogo akitaka aje na uthibitisho,
alafu anasema gari ninayotembela ni yake? gari ni yangu mpaka kazi
ninazo mimi huo ni ujinga na ndio maana siwezi nikaachia hii kitu iende
hivyo hivyo tu kama anavyotaka yeye” – Wema
“Kama kweli ningekua
namchukulia mwanamke wake sidhani kama ningekua nimefikishana nae hapa
tulipofika manake ningekua namuogopa, sasa simuogopi na afanye chochote
anachotaka kufanya, waniache na maisha yangu nimekaa kimya mtoto wa watu
wananifatafata, nikisema watasema nimesema, waniache basi mi mwenyewe
nina maisha yangu ya kuishi” hayo ni maneno ya Wema ambae pia amekataa
na kuapa kwamba hajawahi kutumia bili za milioni 1.5 mpaka mbili kwenye
baa ya huyo mwanamke, huku ikidaiwa kwamba bili hizo zimekua zikilipwa
na huyo pedeshee ambae ni mume wa mwanamke mwenye pub.
Jana mmoja kati ya marafiki wa
Wema akiwa ni mdogo wake na mke wa pedeshee huyo, alikiri kwamba urafiki
wake na Wema umevunjika baada ya kugundua anatoka kimapenzi na mume wa
dada yake (yani mume wa mwanamke aliemfanyia Wema fujo)



No comments