BABA MZAZI WA LULU AFUNGUKA, AOMBA HAKI ITENDEKE KATIKA KESI YA BINTI YAKE
Bw. Michael Edward Kimemeta - Baba Mzazi wa Elizabeth Michel " Lulu"
Elizabeth Michel " Lulu".
Picha, Habari: Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
BABA mzazi wa Muigizaji wa kike wa filamu nchini maarufu kama Lulu,
ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba, ameibuka
na kueleza kushtushwa sana na taarifa za kifo hicho pamoja na habari
kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli
na kuwa anahusika na kifo chake.
Baba Lulu, ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta
(49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro, kaiambia Globu…
Bw. Michael Edward Kimemeta - Baba Mzazi wa Elizabeth Michel " Lulu"
Elizabeth Michel " Lulu".
Picha, Habari: Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
BABA mzazi wa Muigizaji wa kike wa filamu nchini maarufu kama Lulu,
ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba, ameibuka
na kueleza kushtushwa sana na taarifa za kifo hicho pamoja na habari
kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli
na kuwa anahusika na kifo chake.
Baba Lulu, ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta
(49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro, kaiambia Globu ya
Jamii leo huko Moshi kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa
mtoto wake Lulu, lakini hakuamini masikio yake baada ya kupata taarifa
za kifo hicho, huku bintiye, anayedaiwa alikuwa na mahusiano ya
kimapenzi na marehemu, anahusika.
Lulu alifikishwa mahakamani juzi Aprili 11, 2012 akikabiliwa na
mashtaka ya mauaji ya Marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni siku nne baada
ya kifo cha msanii huyo.
Alisema kuwa Elizabeth ama Lulu alizaliwa tarehe April 17,1995 katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, na kwamba
alimaliza elimu ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Midway
mwaka jana na kwamba hivi sasa ana umri wa miaka 17.
Bw. Kimemeta alisema kuwa ni vyema polisi kuwa makini katika
uchunguzi wao kwa kuzingatia kuwa tukio hilo limejenga chuki na uhasama
baina ya Lulu na ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa marehemu Steven
Kanumba.
Alisema kuwa kilichomshtusha zaidi ni taarifa za polisi kusema kuwa
kulitokea ugomvi kati ya Marehemu Steve Kanumba na Lulu, huku ikitajwa
kuwa walikuwa wapenzi.
“Hatukutegemea kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano y
kimapenzi na binti yetu; kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kiasi
kikubwa katika kuendeleza na kukikuza kipaji alichokuwa nacho
Elizabeth”, alisema baba mtu.
“Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuingilia
suala hili na kusaidia katika kupatikana kwa haki dhidi ya shitaka la
mauaji linalomkabili binti yangu Elizabeth na pia naomba swala hili
lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake”
alisema.
Alisisitiza kuwa jamii inatakiwa kutambua mazingira ya tukio hilo,
ambapo chanzo kinasemekana ni ugomvi uliopelekea tafrani kwa Lulu
kutuhumiwa kumsukuma Marehemu Kanumba kwa kile kinachodaiwa kuwa ulikuwa
wivu wa kimapenzi na haiyumkini hakukusudia kumuua hivyo yeye
anashangaa bintiye kuhusishwa moja kwa moja na mauaji.
“Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa nilikwishapata wasiwasi
na mama yake mzazi alikuwa akiwasiliana na Marehemu Kanumba enzi za uhai
wake ambaye alikuwa anamhakikishia usalama wa Lulu na kusema kuwa
ataendelea kubaki kama mwalimu.. lakini leo nasikia alikuwa ni mpenzi -
nilishtushwa” alisema Kimemeta.
Baba Lulu pia ameelezea kusikitishwa kwake kwa kushindwa kuhudhuria
mazishi ya marehemu Steven Kanumba kuhofia usalama wake, na kusema
mazingira yatakaporuhusu hata sitaki kufika nyumbani kwa marehemu Steven
Kanumba na kutoa pole.
Bw. Kimemeta amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa
familia ya Marehemu Steven Kanumba na kutoa mkono wa pole kwa msiba huo
mkubwa ambao haukutarajiwa.
Kasema kuwa Kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri kwenye sanaa na kwamba amecha pengo kwa familia yake na Tanzania kwa ujumla.
Kasema kuwa Kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri kwenye sanaa na kwamba amecha pengo kwa familia yake na Tanzania kwa ujumla.



No comments