CHIDI BENZ AMJINBU AFANDE SELLE ......
Pamoja
na kwamba watu wanaona ni beef imeanza kati ya Afande Selle na Chidi
Beenz, Chidi Beenz amesema wiki moja kabla ya Afande Selle kumdiss on
East Africa Radio, alikua amepanga kumtafuta kwa ajili ya kumpa shavu la
single yake mpya anayotaka zisikike sauti za Mwana FA na Afande Selle.
Amesema
“wiki moja kabla nilikua niko na Tippo wa Zizzou tulikua tunaongelea
ngoma flani hivi niliwahi kurekodi nikaanza kurekodi chorus alafu
nikaiacha, nikamtumia Mwana FA aandike verse yake pia ngoma inaitwa
Mani, Zizzou akaniambia ukimtumia na Afande itakua poa anaweza kuandika
kitu kizuri sana alafu hajasikika siku nyingi itakua safi, nikasema
kweli bwana hata mimi sijamsikia Afande zamani itabidi nikifika Dar
nimtafute kwenye simu”
Mfalme
wa Ilala amesema “yani juzi nimesikia Afande ananidiss nikacheka,
nikaona Afande juzi tu tumekutana kwenye show ya CLOUDS nimemuona Afande
anazurura peke yake nikamuita nikiwa na Fid Q, Prof J, FA na wengine
nikamwambia Afande njoo tupige picha mpaka leo ninayo, watu walicheka
wakafurahi pia, sasa from no where Afande amenidiss mimi wakati mi
sijawahi kusema chochote kibaya kuhusu yeye”
Kwa
kumalizia CHIDI amesema “sijaufuta huo mpango wa kufanya kolabo na
Afande Selle, namfahamu ni mtu mmoja anabadilika kwa haraka sana na
kuomba sana msamaha, wazo la kufanya nae kolabo bado ninalo na kama
atakubali tutarekodi, hakuna sababu ya kugombana wala kusemana”
Chanzo
cha haya yote ni wakati Afande Selle alipofananisha kitendo cha
mwimbaji DITTO kuondoka kwenye kundi lake la WATU PORI na kwenda LA
FAMILIA ya CHIDI BENZ, sawa na kuondoka MANCHESTER UNITED kwenda
WOLVERMPTON.
Akiamplfy
na millardayo.com march 26 2012, Chidi alikanusha taarifa kwamba
atamteka na kumpiga Afande Selle vilevile akamuonya JAY MOE kutoingilia
chochote kati yake na Afande Selle huku akisisitiza kwamba “hata
nilivyomuona na Jay Moe kwenye ile interview namuona Jay Moe, Jay Moe ni
nini bwana vitu anaongea Jay Moe pale na Afande wote kabila moja, ni
watu ongea sawa”
Chidi
amesema hatofanya chochote kama ikitokea akakutana na Afande Selle
sehemu yoyote, atamsalimia na kuendelea na shughuli nyingine.



No comments