UKWELI KUHUSU DULLY SYKES KUKAMATWA NA POLISI.........
Inawezekana
uliwaza labda kampa mimba mwanafunzi, kaiba, kapigana? Kamtukana mtu?
Hayo yote inawezekana yaliku majibu yako, na kama ndio hivyo….
Haujapatia kwa sababu ukweli wenyewe, Dully kaamua kuuweka wazi.
Dully
amesema “nilikua naelekea mjini kusaini mkataba wa tangazo la pombe
sasa kufika pale keko kumbe kulikua na msafara wa Rais anaelekea
Airport, sasa kufika pale jamaa mwenye pesa yangu ya tangazo akasema
anataka kusepa kwa hiyo akili yangu ikawa inawaza kuwahi, kumbe askari
alikua amenizuia nikataka kumgonga, akawa ananizuia nikaona sasa huu
umeshakua msala, ikabidi nikimbie niende keko nikakutana na foleni
ikabidi niingie kwenye petrol station, nikasimama nikazima gari,
nikashuka”
Dully
amesema “polisi walinizingira kabla na kuanza kukoki mabastola yao,
polisi wengine wakaongezeka na defender, nikashuka kwenye gari ikabidi
niongee nao kwa hiyo nikawaambia mi nawahi sehemu ikabidi waniambie basi
subiri msafara wa rais upite tutakuachia, hata hivyo walinikuta na
makosa mawili ambayo waliniandikia, nilikua sina leseni niliacha
nyumbani na kosa jingine ni insuarance yangu kuisha, hakuna kingine
zaidi ya hapo”



No comments