Je! Beef hii ni Dar dhidi ya Arusha?
“These
rap cats softer than a new born baby bottom... Eti big fish in this
ocean... My pussy cat eats that shit..” Ni maneno yanayosemeka katika
ukuta (wall) wa Harry Kaale maarufu kwa jina la One The Incredible aka
Moko wa Miujiza. Ni fataki alilolielekeza kwa Joh Makini kuashiria kuwa
vita katika ya Weusi kundi huru linalojumuisha rappers kutoka Arusha
ambao ni yeye mwenyewe Joh, nduguye Nikki wa Pili, Gnako, Bonta aka
Maarifa, Lord Eyez na wengine dhidi ya Nikki Mbishi aka Baba Malcom na
One the Incredible na washirika wengine wa Lunduno na Illmatic imeiva.
Chanzo
cha ugomvi huu wa kimuziki kati ya pande hizi mbili unaaminika kuanza
katika kipindi cha mwaka mmoja na kitu uliopita. Katika mazingira mengi
ya kuzuka kwa beef za hiphop mashabiki huwa na asilimia nyingi za kwao
zinazopelekea wasanii fulani kupaniana kiushindani hali inayosababisha
beef ya kawaida ama kali. Jina la “Nikki”ni sehemu moja wapo ya kuwepo
kwa tension kati ya Nikki wa Pili na Nikki Mbishi. Watu walianza
kumsikia kwa ukamilifu Nikki wa pili katika wimbo alioimba na ndugu yake
Joe Makini “Niaje ni Vipi” . Hapo ndipo mashabiki wa hiphop Bongo
wakatambua kuongezeka rasmi kwa orodha ya wasanii wenye uwezo mzuri
kiuandishi nchini wanaotokea Arusha. Baadaye Nikki wa Pili alisimama
mwenyewe kwenye ngoma aliyomshirikisha Rama D “Good Boy”.
Kwa
upande wa Nikki Mbishi, safari yake ya kuwa nyota katika hiphop ilikuwa
tofauti kidogo. Yeye alianza kujulikana nchini kabla hata hajaachia
wimbo uliorekodiwa na kusambazwa katika mkondo mkuu wa muziki wa
Tanzania. Nikki Mbishi alijizolea umaarufu katika kipindi cha Bongo
Flava cha Clouds Fm kwa uwezo wake wa kuchana ,mitindo huru
(Freestyles). Kwa mujibu wa watu wanaomfahamu kwa ukaribu, wanasema
Nikki Mbishi ana uwezo wa kurap kwa freestyle kwa masaa kadhaa bila
kurudia mada na ndiye msaani ambaye One anamhofia kuliko wote nchini.
Baada
ya kuvikwa taji la mchanaji bora wa mitindo huru enzi hizo, Nikki
Mbishi aliongezea msumari mzito kwa mashabiki wake katika wimbo wake wa
“Punch za kwenye Line” Kama jina la wimbo unavyojieleza, wimbo mzima
ulijaa uandishi mzito unaohitaji muda mrefu kuchambua na kupata maana
halisi ya kila alichokuwa anatema (spit), sifa ambayo imekuwa ikipelekwa
pia kwa maswahiba wake One na Stereo. Mashabiki wa wasanii hawa
wanaofanana majina ya mwanzo wakawa na shauku ya kujua uwezo wa kila
mmoja ili kupata jibu na ni mkali zaidi ya mwenzie. Jibu wanalo
mashabiki wenyewe. Lakini hapo ndipo story hii iliyotawala vinywa vya
mashabiki wa hiphop nchini, vituo vya radio na mijadala katika mitandao
ya kijamii kwa sasa kuhusu beef kati ya Weusi na Nikki Mbishi na One
ilipopandikiza mbegu zake.
Kwa
mujibu wa story za chini kwa chini ni kwamba Nikki Mbishi
alimshirikisha Rama D kwenye chorus ya Punch za Kwenye Line lakini
baadaye Rama D akaomba kuondolewa sauti zake kwenye wimbo huo kwakuwa
hakutaka kugombana na Joh Makini ambaye inasemekana hakuwa anampenda
Nikki Mbishi. Kutokana na uamuzi huo wa Rama D, Duke ambaye ndo producer
wa wimbo huo pamoja na uongozi wa MLAB wakaamua kumchukua Grace Matata
kufanya chorus. Kwao MLAB huo ulikuwa ni uamuzi uliofanyika kwa
kutopenda kwakuwa Grace kipindi hicho alikuwa bado msaani mchanga na
asiyejulikana kwa wengi kama ilivyo sasa.
Baada
ya hatua hiyo kukaanza kuzuka maneno kutoka kwenye kambi ya River Camp
Soldiers na kuonekana kuwepo uwezekano wa kambi hiyo kuwadiss Lunduno
(kundi huru lililopo maskani wanapotokea Stereo na nikki ambao kwa sasa
wamejitoa). Kambi ya Lunduno kupitia One ikatupa jiwe lake kuelekeza kwa
River Camp soldiers ambao kwa sasa wapo ndani ya kundi kubwa
linalowajumuisha pia member wa Nako 2 Nako liitwalo “Weusi”.
Kwa
mujibu wa mahojiano na Clouds FM, One alidai kuwa alirekodi wimbo
katika studio za Tongwe Records ambayo kuna mstari unasema siwezi kuuza
kura yangu kama Bonta akimaanisha wimbo wa Bonta uitwao “Nauza Kura”.
Pamoja na dongo hilo lililoekezwa kwa Bonta, hakuna jibu la wazi kutoka
kwa Bonta zaidi ya kujibu “Sina tofauti nao” alipoulizwa kuhusu msimamo
wake.
Katika
mahojiano hayo One alisema anashangaa kujikuta yupo kwenye beef na
Weusi wakati anawasiliana mara kwa mara na Joh Makini pamoja na Lord
Eyez ambao kwake ni kama kaka zake kimuziki. Japokuwa kauli hii ya One
inakinzana na status yake hapo mwanzoni kabisa mwa makala haya ambapo
anamdiss wazi wazi Joh Makini.
Mahojiano
hayo yalifanyika kutaka kuwepo ufafanuzi kuhusiana na status ya
facebook aliyoiweka jumatano (28/03/2012) iliyosema: “Niki wa pili:
sijakutaja, usijihusishe, this is none of your biz..Do you homo…”
One
alifafanua kuwa sababu ya kuandika status hiyo ni kutokana na hatua ya
Nikki wa pili kumtumia ujumbe Nikki Mbishi ambao Mbishi alimfowadia
ukisema kuwa wao akina One bado ni wadogo kwenye muziki na hawawezi rap,
pia album ya Mbishi inasound kama single moja.
Kuhusu
namna anavyowachukulia members wa Weusi, One anasema “Ni wazi kuwa
siwakubali Weusi, si kama nawakosea heshima bali ni jibu nitakalokupa
kama ukiniuliza kama shabiki, mimi si shabiki wao, Ujue nina waheshimu
wao kama kundi lenye mafanikio kulingana na kile wanachofanya, hivyo
hiyo ni heshima kubwa niliyonayo kwao lakini mimi si shabiki wao”
(phatbeattz.blogspot.com).
Nikki
Mbishi pia ameonesha wazi kutomkubali Bonta kama msanii hali
inayoashiria kuwa ni ngumu kwa Bonta ama Weusi kwa ujumla kukaa kimya;
“Ninaposema Bonta hayupo conscious namaanisha kuwa naheshimu
anachofanya, ana ujumbe wa maana lakini uwasilishaji wa ujumbe wake kwa
umma ndio tatizo. Kwa neno moja naweza kusema Bonta ni MC mbovu,na
ninaposema hivyo namaanisha kuwa hajui kurap, anachofanya nikuongea na
wakati mwingine anapata beat nzuri za kuongelea. Nadhani huu ni muda wa
kuwaambia ukweli” (phatbeattz.blogspot.com)
Hata
hivyo kama mwenzie One, Nikki Mbishi pia ameonesha wazi kung’ata na
kupuliza kuhusiana na suala hili “if my mind is a belly then am bellyful
I don't think if there is a space to put this cow meat a.k.a
BEEF......”
Tayari
mashabiki wa pande zote mbili wameanza kujihusisha moja kwa moja kwa
kutoa mawazo yao katika kurasa za wasanii hao. “Tunachoshindwa kuelewa
wabongo siku zote ni hiki.., Ukweli haui-justified kwa pesa, umaarufu na
ujanja ujanja wa maneno. Muziki utabaki kuwa Muziki. Hip Hop itabaki
kuwa Hip Hop. Kama "samaki Kwenye Hii Bahari" atazingua.., "tunamvua" tu
kwani niaje...!? SUPPORT KWA Nikki Mbishi BabaMalcom NA WOTE
WANAOSIMAMA FOR HIP HOP!!!”
Wengine
wameshindwa kuzuia chuki zao na kuandika maneno makali dhidi ya Weusi
kuonesha namna wanavyoiunga mkono kambi ya akina Nikki Mbishi.
“Watajichubua tu hao weusi. Watoto wazuri wanajiita weusi, hatutaki
matozi. One, stereo na Nikki Mbishi wana big screen inayoönyesha u2po wa
mabitch weusi. One wagonge ta**o, Nikki mbishi, wachinje huku
wanakuchea, stereo watie vitasa watoto wanazingua”.
Vyombo
vya habari husasan radio ambavyo siku zote vinaongoza kwa kukuza beef
za aina hii vimechukua nafasi zao kwa kufanya mahojiano kupata ufafanuzi
juu ya suala lenyewe hali inayolikuza zaidi.
MLAB
ambayo ni nyumbani kwa One, Nikki Mbishi na Stereo imeonesha
kutofurahishwa na beef hiyo inayoendelea kukua kwa kasi. Meneja wa
wasanii na Studio wa MLAB Patrick Gondwe amemuomba Nikki Mbishi kuachana
na beef hiyo. “ Kama kaka, nakuomba kuachana na suala hili Nikki!
Kambi zote mbili ziache kuwagawa mashabiki…..Wapo kwa ajili yetu na hilo
ni suala muhimu… Hatutakiwi kutawaliwa na vyombo vya habari.. Siku zote
habari mbaya ni habari njema kwao….kutatokea mengi ya kuchanganya
lakini mwisho wa siku sisi tutapoteza mara mbili. Tukubali kukosa
(lose) kwa kutokuandika vitu hasi kwenye mitandao ya kijamii na kuziba
midomo yetu dhidi vyombo vya habari kuhusu suala hili. Nakuomba sana”
Uamuzi
wa kukaa kimya kwa pande zinazohitirafiana unaweza kuwa na faida na
hasara. Faida ni kuwa mashabiki wa pande zote mbili watapata fursa ya
kuujua ukweli wa jambo lenyewe na kutafakari. Kwao Weusi na akina Nikki
Mbishi wanaweza kutumia mahojiano na vyombo vya habari kuzuia kuwagawa
mashabiki wao. Hasara ni pale ambapo pande hizi zitajikuta zikitumiwa na
radio ama watu wenye lengo la kufanya biashara kupitia mgongo wao.
Mfano halisi ni jinsi Darlive ilivyotumia beef ya Roma na Izzo
kibiashara.
Kama
beef hii ikiendelea kukua madhara yake yataenda mbali zaidi ya hapa
ilipo. Beef hii inahusisha wasanii wanaowakilisha mikoa mikubwa yenye
ushindani katika muziki wa hiphop, Arusha na Dar es Salaam. Kwa muda
mrefu Arusha imekuwa ikitajwa kuwa ngome imara kwa hiphop nchini hivyo
beef hii inatoa picha ya wazi ya ushindani kati ya Arusha na Dar es
Salaam.
Hatari
ni pale mashabiki wa pande hizi mbili wakigawanyika katika misingi ya
kimkoa. Ikiwa hivyo itakuwa ngumu kwa wasanii kama One, Nikki Mbishi na
Stereo kwenda Arusha kufanya show wakihofia usalama wao. Historia ya
mkoa wa Arusha inatueleza ni kwa kiasi gani watu wa huko walivyo na
ushirikiano katika kupinga kitu wasichokipenda. Japo katika hiphop beef
zina umuhimu wake, tuombee Mungu beef hii isije kufikia hatua ya watu
kupigana wanted katika maskani zao bali kuwapa hasira za kiuandishi wote
wanaohusika na mwisho wa siku kuwapa mashabiki muziki mzuri.
Fredrick Bundala aka Skywalker
Tone Radio


No comments