JE! BEEF HII NI YA DAR DHIDI YA ARUSHA!!!!!!?
“These rap cats softer than a new
born baby bottom... Eti big fish in this ocean... My pussy cat eats that
shit..” Ni maneno yanayosemeka katika ukuta (wall) wa Harry Kaale
maarufu kwa jina la One The Incredible aka Moko wa Miujiza. Ni fataki
alilolielekeza kwa Joh Makini kuashiria
kuwa vita katika ya Weusi kundi huru linalojumuisha rappers kutoka
Arusha ambao ni yeye mwenyewe Joh, nduguye Nikki wa Pili, Gnako, Bonta
aka Maarifa, Lord Eyez na wengine dhidi ya Nikki Mbishi aka Baba Malcom
na One the Incredible na washirika wengine wa Lunduno na Illmatic
imeiva. Chanzo cha ugomvi huu wa kimuziki kati ya pande hizi mbili
unaaminika kuanza katika kipindi cha mwaka mmoja na kitu uliopita.
Katika mazingira mengi ya kuzuka kwa beef za hiphop mashabiki huwa na
asilimia nyingi za kwao zinazopelekea wasanii fulani kupaniana
kiushindani hali inayosababisha beef ya kawaida ama kali. Jina la
“Nikki”ni sehemu moja wapo ya kuwepo kwa tension kati ya Nikki wa Pili
na Nikki Mbishi. Watu walianza kumsikia kwa ukamilifu Nikki wa pili
katika wimbo alioimba na ndugu yake Joe Makini “Niaje ni Vipi” . Hapo
ndipo mashabiki wa hiphop Bongo wakatambua kuongezeka rasmi kwa orodha
ya wasanii wenye uwezo mzuri kiuandishi nchini wanaotokea Arusha.
Baadaye Nikki wa Pili alisimama mwenyewe kwenye ngoma aliyomshirikisha
Rama D “Good Boy”. Kwa upande wa Nikki Mbishi, safari yake ya kuwa nyota
katika hiphop ilikuwa tofauti kidogo. Yeye alianza kujulikana nchini
kabla hata hajaachia wimbo uliorekodiwa na kusambazwa katika mkondo mkuu
wa muziki wa Tanzania. Nikki Mbishi alijizolea umaarufu katika kipindi
cha Bongo Flava cha Clouds Fm kwa uwezo wake wa kuchana ,mitindo huru
(Freestyles). Kwa mujibu wa watu wanaomfahamu kwa ukaribu, wanasema
Nikki Mbishi ana uwezo wa kurap kwa freestyle kwa masaa kadhaa bila
kurudia mada na ndiye msaani ambaye One anamhofia kuliko wote nchini.
Baada ya kuvikwa taji la mchanaji bora wa mitindo huru enzi hizo, Nikki
Mbishi aliongezea msumari mzito kwa mashabiki wake katika wimbo wake wa
“Punch za kwenye Line” Kama jina la wimbo unavyojieleza, wimbo mzima
ulijaa uandishi mzito unaohitaji muda mrefu kuchambua na kupata maana
halisi ya kila alichokuwa anatema (spit), sifa ambayo imekuwa ikipelekwa
pia kwa maswahiba wake One na Stereo. Mashabiki wa wasanii hawa
wanaofanana majina ya mwanzo wakawa na shauku ya kujua uwezo wa kila
mmoja ili kupata jibu na ni mkali zaidi ya mwenzie. Jibu wanalo
mashabiki wenyewe. Lakini hapo ndipo story hii iliyotawala vinywa vya
mashabiki wa hiphop nchini, vituo vya radio na mijadala katika mitandao
ya kijamii kwa sasa kuhusu beef kati ya Weusi na Nikki Mbishi na One
ilipopandikiza mbegu zake. Kwa mujibu wa story za chini kwa chini ni
kwamba Nikki Mbishi alimshirikisha Rama D kwenye chorus ya Punch za
Kwenye Line lakini baadaye Rama D akaomba kuondolewa sauti zake kwenye
wimbo huo kwakuwa hakutaka kugombana na Joh Makini ambaye inasemekana
hakuwa anampenda Nikki Mbishi. Kutokana na uamuzi huo wa Rama D, Duke
ambaye ndo producer wa wimbo huo pamoja na uongozi wa MLAB wakaamua
kumchukua Grace Matata kufanya chorus. Kwao MLAB huo ulikuwa ni uamuzi
uliofanyika kwa kutopenda kwakuwa Grace kipindi hicho alikuwa bado
msaani mchanga na asiyejulikana kwa wengi kama ilivyo sasa. Baada ya
hatua hiyo kukaanza kuzuka maneno kutoka kwenye kambi ya River Camp
Soldiers na kuonekana kuwepo uwezekano wa kambi hiyo kuwadiss Lunduno
(kundi huru lililopo maskani wanapotokea Stereo na nikki ambao kwa sasa
wamejitoa). Kambi ya Lunduno kupitia One ikatupa jiwe lake kuelekeza kwa
River Camp soldiers ambao kwa sasa wapo ndani ya kundi kubwa
linalowajumuisha pia member wa Nako 2 Nako liitwalo “Weusi”. Kwa mujibu
wa mahojiano na Clouds FM, One alidai kuwa alirekodi wimbo katika
studio za Tongwe Records ambayo kuna mstari unasema siwezi kuuza kura
yangu kama Bonta akimaanisha wimbo wa Bonta uitwao “Nauza Kura”. Pamoja
na dongo hilo lililoekezwa kwa Bonta, hakuna jibu la wazi kutoka kwa
Bonta zaidi ya kujibu “Sina tofauti nao” alipoulizwa kuhusu msimamo
wake. Katika mahojiano hayo One alisema anashangaa kujikuta yupo kwenye
beef na Weusi wakati anawasiliana mara kwa mara na Joh Makini pamoja na
Lord Eyez ambao kwake ni kama kaka zake kimuziki. Japokuwa kauli hii ya
One inakinzana na status yake hapo mwanzoni kabisa mwa makala haya
ambapo anamdiss wazi wazi Joh Makini. Mahojiano hayo yalifanyika kutaka
kuwepo ufafanuzi kuhusiana na status ya facebook aliyoiweka jumatano
(28/03/2012) iliyosema: “Niki wa pili: sijakutaja, usijihusishe, this is
none of your biz..Do you homo…” One alifafanua kuwa sababu ya
kuandika status hiyo ni kutokana na hatua ya Nikki wa pili kumtumia
ujumbe Nikki Mbishi ambao Mbishi alimfowadia ukisema kuwa wao akina One
bado ni wadogo kwenye muziki na hawawezi rap, pia album ya Mbishi
inasound kama single moja. Kuhusu namna anavyowachukulia members wa
Weusi, One anasema “Ni wazi kuwa siwakubali Weusi, si kama nawakosea
heshima bali ni jibu nitakalokupa kama ukiniuliza kama shabiki, mimi si
shabiki wao, Ujue nina waheshimu wao kama kundi lenye mafanikio
kulingana na kile wanachofanya, hivyo hiyo ni heshima kubwa niliyonayo
kwao lakini mimi si shabiki wao” (phatbeattz.blogspot.com). Nikki
Mbishi pia ameonesha wazi kutomkubali Bonta kama msanii hali
inayoashiria kuwa ni ngumu kwa Bonta ama Weusi kwa ujumla kukaa kimya;
“Ninaposema Bonta hayupo conscious namaanisha kuwa naheshimu
anachofanya, ana ujumbe wa maana lakini uwasilishaji wa ujumbe wake kwa
umma ndio tatizo. Kwa neno moja naweza kusema Bonta ni MC mbovu,na
ninaposema hivyo namaanisha kuwa hajui kurap, anachofanya nikuongea na
wakati mwingine anapata beat nzuri za kuongelea. Nadhani huu ni muda wa
kuwaambia ukweli” (phatbeattz.blogspot.com) Hata hivyo kama mwenzie
One, Nikki Mbishi pia ameonesha wazi kung’ata na kupuliza kuhusiana na
suala hili “if my mind is a belly then am bellyful I don't think if
there is a space to put this cow meat a.k.a BEEF......” Tayari
mashabiki wa pande zote mbili wameanza kujihusisha moja kwa moja kwa
kutoa mawazo yao katika kurasa za wasanii hao. “Tunachoshindwa kuelewa
wabongo siku zote ni hiki.., Ukweli haui-justified kwa pesa, umaarufu na
ujanja ujanja wa maneno. Muziki utabaki kuwa Muziki. Hip Hop itabaki
kuwa Hip Hop. Kama "samaki Kwenye Hii Bahari" atazingua.., "tunamvua" tu
kwani niaje...!? SUPPORT KWA Nikki Mbishi BabaMalcom NA WOTE
WANAOSIMAMA FOR HIP HOP!!!” Wengine wameshindwa kuzuia chuki zao na
kuandika maneno makali dhidi ya Weusi kuonesha namna wanavyoiunga mkono
kambi ya akina Nikki Mbishi. “Watajichubua tu hao weusi. Watoto wazuri
wanajiita weusi, hatutaki matozi. One, stereo na Nikki Mbishi wana big
screen inayoönyesha u2po wa mabitch weusi. One wagonge ta**o, Nikki
mbishi, wachinje huku wanakuchea, stereo watie vitasa watoto
wanazingua”. Vyombo vya habari husasan radio ambavyo siku zote
vinaongoza kwa kukuza beef za aina hii vimechukua nafasi zao kwa kufanya
mahojiano kupata ufafanuzi juu ya suala lenyewe hali inayolikuza zaidi.
MLAB ambayo ni nyumbani kwa One, Nikki Mbishi na Stereo imeonesha
kutofurahishwa na beef hiyo inayoendelea kukua kwa kasi. Meneja wa
wasanii na Studio wa MLAB Patrick Gondwe amemuomba Nikki Mbishi kuachana
na beef hiyo. “ Kama kaka, nakuomba kuachana na suala hili Nikki! Kambi
zote mbili ziache kuwagawa mashabiki…..Wapo kwa ajili yetu na hilo ni
suala muhimu… Hatutakiwi kutawaliwa na vyombo vya habari.. Siku zote
habari mbaya ni habari njema kwao….kutatokea mengi ya kuchanganya lakini
mwisho wa siku sisi tutapoteza mara mbili. Tukubali kukosa (lose) kwa
kutokuandika vitu hasi kwenye mitandao ya kijamii na kuziba midomo yetu
dhidi vyombo vya habari kuhusu suala hili. Nakuomba sana” Uamuzi wa
kukaa kimya kwa pande zinazohitirafiana unaweza kuwa na faida na hasara.
Faida ni kuwa mashabiki wa pande zote mbili watapata fursa ya kuujua
ukweli wa jambo lenyewe na kutafakari. Kwao Weusi na akina Nikki Mbishi
wanaweza kutumia mahojiano na vyombo vya habari kuzuia kuwagawa
mashabiki wao. Hasara ni pale ambapo pande hizi zitajikuta zikitumiwa na
radio ama watu wenye lengo la kufanya biashara kupitia mgongo wao.
Mfano halisi ni jinsi Darlive ilivyotumia beef ya Roma na Izzo
kibiashara. Kama beef hii ikiendelea kukua madhara yake yataenda mbali
zaidi ya hapa ilipo. Beef hii inahusisha wasanii wanaowakilisha mikoa
mikubwa yenye ushindani katika muziki wa hiphop, Arusha na Dar es
Salaam. Kwa muda mrefu Arusha imekuwa ikitajwa kuwa ngome imara kwa
hiphop nchini hivyo beef hii inatoa picha ya wazi ya ushindani kati ya
Arusha na Dar es Salaam. Hatari ni pale mashabiki wa pande hizi mbili
wakigawanyika katika misingi ya kimkoa. Ikiwa hivyo itakuwa ngumu kwa
wasanii kama One, Nikki Mbishi na Stereo kwenda Arusha kufanya show
wakihofia usalama wao. Historia ya mkoa wa Arusha inatueleza ni kwa
kiasi gani watu wa huko walivyo na ushirikiano katika kupinga kitu
wasichokipenda. Japo katika hiphop beef zina umuhimu wake, tuombee Mungu
beef hii isije kufikia hatua ya watu kupigana wanted katika maskani zao
bali kuwapa hasira za kiuandishi wote wanaohusika na mwisho wa siku
kuwapa mashabiki muziki mzuri. Fredrick Bundala aka Skywalker Tone
Radio



No comments