ALICHOKISEMA MBUNGE HALIMA MDEE KUHUSU MWIGIZAJI LULU.
Halima Mdee
Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA
Halima Mdee amekiri kwamba kuna baadhi ya watu waliopinga au
kutofautiana nae baada yakutangaza uamuzi wa kumsadia mwigizaji LULU
ambae sasa hivi yuko gerezani SEGEREA kwa tuhuma za mauaji ya mwigizaji
STEVEN KANUMBA.
Amesema “kitu ambacho
nimefarijika ni kwamba kama kuna watu 50 wanaotoa comments basi arobaini
zitakua zinasupport, na 10 zitaponda na ni kitu ambacho ni cha kawaida
sana kwa sababu kila mtu anatafsiri kivyake”
Halima amesema “kweli nimeguswa
sana na msiba wa Kanumba, kilichonifanya kwenda kumuona Lulu akiwa
chini ya ulinzi wa polisi na nikakutana pia na mama yake nikajua kwamba
inawezekana kabisa kuna upande wa pili wa hadithi ambao unahitaji sauti
yake kusikika kwa sababu wengi katika hatua za mwanzo tumemuhukumu sana
ikizingatiwa kwamba ni mtoto mdogo, nikashawishika tu kwenda kutaka
kujua kwa sababu na mimi nilikua simjui, namsoma tu kwenye magazeti”
Mdee
amesema “siwezi kusema kwamba hajafanya kosa, hapana kwa sababu hakuna
mtu aliekuepo zaidi ya hao wawili na pia nikagundua kwamba ni mtu ambae
ana uhitaji sasa hivi hasa ukizingatia umri wake, kumbe pamoja na utoto
wake familia yake ndio ilikua inamtegemea yeye, tunajua kesi kama hizi
ambazo zina presha kubwa sana ya umma, tunaweza kujikuta kwamba ule
ukweli halisi ambao ungeweza ukajulikana unaweza kuzuiwa kujulikana kwa
sababu ya presha ya Umma”
“Kimsingi sitaki kulizungumza
sana hili ili nisiingilie maswala yanayoendelea mahakamani lakini
tulivyoenda bahati nzuri walikuwepo hata baadhi ya maofisa wa polisi
ambao walisema kabisa kwamba jana yake Lulu alipelekwa hospitali
kuchunguzwa kama vile vipigo alivyokua akipewa viliweza kumuathiri
ndani, kwa maelezo yake yeye ni kwamba alikua anapigwa kwa ubapa wa
panga”




No comments