Breaking News

NIMPENDE NAN YA DIAMOND KUONEKANA VIDEONI…........


MSANII wa muziki wa kizazi bongo Nassib Abdul ‘Diamond’, amesema kuwa April 20 mwaka huu, itakuwa ni siku maalum kwake kwani atakuwa anaitambulisha video ya wimbo wake wa ‘Nimpende Nani’.

Wimbo huo umefanya vizuri na kuwa gumzo kubwa ndani ya jamii kwani baadhi ya mashabiki wake walihisi ngoma hiyo ni swali kwao ili wampe jibu kati ya Wema Sepetu na Jokate, ampende nani lakini haupo katika mtazamo huo.

Msanii huyo alisema kuwa kufanya vizuri kwa wimbo huo ndiko kuliko mpa hamasa ya kutoa video yake kwani anaamini hata hiyo itafanya vizuri.

“April 20 mwaka huo video yangu itakuwa sokoni hivyo nawaomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwani siku si nyingi wataona ukweli wote unaopatikana ndani ya wimbo huo,” alisema.

Hata hivyo msanii huyo wa nyimbo ‘Mbagala’, aliongeza kuwa Ijumaa ya wiki hii atakuwa na shoo kubwa kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

Lengo kubwa la kufanya shoo hiyo ni kuwakutanisha watu hasa viongozi ambao wamekuwa wakitamani kushuhudia matamasha yake lakini wanakosa kutokana na mazingira eneo ambayo wao hawezi kuigia lakini kwa hapo anaamini watahudhuria kwa wingi.

“Mlimani City kutakuwa kama Ulaya siku hiyo kwa sababu ndani ya ukumbi huo kutakuwa kama kumbi ambazo wasanii wa Marekani wanakofanyia shoo zao hivyo nawaomba watu waje kushuhudia nini kitakachofanyika kwa sababu itakuwa ni siku pekee kwao kuona utofauti kwani nitakuwa na wacheza shoo zaidi ya 25.” Alisema Diamond Platnumz

No comments