Breaking News

MIZIMU YA BABA INANISAIDIA.......


MWIGIZAJI Gwyneth Paltrow, amesema huwa anaongea na mzimu wa baba yake kupitia pete yake ya ndoa aliyopewa kama urithi.

Anasema mara zote anapokuwa na jambo ambalo anaamini anahitaji usaidizi wa baba yake, huwa anaongea na pete hiyo na shida yake hutatuka.

"Ninaamini mtu akifa mzimu wake unabaki ukiishi, ndiyo maana mara zote nikiishika pete ya baba na kuanza kuzungumza, huwa ninahisi kabisa yupo karibu yangu, hata harufu ya manukato aliyokuwa akitumia huwa nayasikia," anasema Paltrow.
Baba yake (Bruce Paltrow) alifariki nchini Ufaransa mwaka 2000 kwa ugonjwa wa kansa ya koo, siku chache baada ya Gwyneth kushinda Tuzo ya Oscar.
Hii si mara ya kwanza kwa mwigizaji huyo kusema anaona mizimu ya wafu, mwaka 2006 alisema alikuwa akiuona mzimu wa mwanamuziki, Adolphus White, aliyekuwa akiishi katika nyumba waliyoinunua huko England.

No comments