Breaking News

RIHANNA ACHANWA HADHARANI.....


INGAWA mwanamuziki Rihanna anaaminika kuwa mwenye mafanikio na mwenye kujituma jukwaani, wapo ambao wanaamini kuwa mwanamuziki huyo hastahili sifa hizo kwa kuwa muziki wake haukidhi viwango.

Mwanamuziki Gene Simmons amesema wazi katika mkutano na waandishi wa habari kuwa Rihanna ni mmoja kati ya wanamuziki wanaohitaji mafunzo ya kuburudisha na kuimba kwa kuwa bado mchanga katika tasnia hiyo.

"Tumechoka kuwaona wanamuziki wakipanda majukwaani na wacheza shoo huku nyuma yao CD ikiwasaidia kuimba, wakati huo umepitwa," alisema Simmons.

Aliongeza kuwa wasanii wote wakali wanapaswa kupiga muziki wao moja kwa moja na si kutumia CD kama mastaa wengi wanavyofanya duniani, akiwemo Rihanna.

Simmons anasema kuliko aende kwenye shoo ya Rihanna ni bora aangalie kipindi cha American Idol kwa kuwa wanaimba kwa kutumia vyombo moja kwa moja.

No comments