Breaking News

Ngosha Atunukiwa Cheti Na Under The Same Sun...


Mkali wa mashahiri na flow kalitoka Mwanza Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q ametunukiwa cheti maalum na shirika linalosaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) linalojulikana kama Under The Same Sun, kwa mchango wake mkubwa katika ku-support campaign ya shirika hilo.
        Ngosha aliweka picha [hapo juu] kupitia ukurasa wake wa Facebook na kuandika ''Just received a Certificate of Appreciation from the one and only Mr.Peter Ash (CEO of Under The Same Sun)''.
       Mwaka jana, rapper Fid Q akiwa na wasanii wengine wa kizazi kipya walizungukia mikoa tofauti pamoja na kanda ya ziwa kupinga mauaji ya Albino wakiwa na shirika hilo. Baada ya miezi kadhaa walirudi tena mikoa ya kanda ya ziwa kuwashukuru wakazi wa kanda ya ziwa kwa sababu mauaji ya walemavu hawa wa ngozi yalipungua sana hivyo campaign yao ya kushirikiana na wakazi wa kanda ya ziwa ilifanikiwa. 

No comments