Breaking News

Neno la Lord Eyez na Fid Q

Karibia kila kukicha kuna kitu kinatokea ambacho kinaashiria kuwa TZhiphop inazidi kukomaa. Binafsi sielewi wale ambao bado wanadai Hip Hop ya Bongo imekufa. Labda kinachopaswa kufanywa ni mashabiki kuongeza juhudi za kusaka nyimbo makini za Hip Hop — ukichimba kidogo tu utakutana na nyimbo kibao!
Na leo nina haki ya kutambulisha huu wimbo kama mmoja wa mashabiki wakubwa wa Nako 2 Nako na Fid Q; kasoro iliyopo kwenye wimbo huu ni moja tu — G-Nako hayupo. Ila kama kawaida, Lord Eyez anatambaa na beat kama hataki huku akibadilishana bars na Fid Q.

No comments