Breaking News

WEMA + DIAMOND =ZEROOOOOOOOOOOO


 Na Luquman Maloto
NUNGE mbili zikijumlishwa, bado jibu linabaki kuwa ziro! Uhusiano wa kimapenzi kati ya 'Bwamdogo' anayeimba Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond' na shugamami wake, Wema Sepetu, umekutanisha sifuri wawili.

‘Bi mkubwa’ Wema aliyebahatika kupewa taji la Miss Tanzania 2006/07 na ‘bwa mdogo’ Diamond wanatisha kwa sasa mtandaoni kwa picha za mapozi ya kingono, hivyo kuonesha kuwa wawili hao wakiwa pamoja, hutumia muda wao mwingi ‘kuchakachua’ na kubadili mitindo ya ‘mafoto’.

The 5star Paper, Risasi Jumamosi lina jumla ya picha zaidi ya 74 ambazo limezikusanya kutoka vyanzo mbalimbali, zikiwaonesha ‘Serengeti Boy’ Diamond na ‘Shugamami’ Wema katika mapozi ya ndani zaidi ya kimahaba.

Pamoja na ukweli kwamba nyingi kati ya picha hizo zinafanana kutoka mtandao mmoja hadi mwingine, jinsi zilivyosambaa ni ishara kuwa wawili hao wapo ‘bize’ katika kutekeleza jambo moja kila siku.

USANII WA DIAMOND
Rekodi zinaonesha kuwa bwa mdogo Diamond kila anapoulizwa kuhusu uhusiano wake na Wema, amekuwa mgumu kujibu kwa madai kwamba akil
i yake ameielekeza katika kazi yake ya muziki.

Hata hivyo, Risasi Jumamosi linaweza kuthibitisha kwa picha kwamba pamoja na ‘ubize’ alionao kwenye kazi zake za muziki, Diamond pia yupo kwenye ‘resi’ katika mapenzi hasa baada ya kujiweka kwa bi mkubwa Wema.

Aidha, picha hizo zinathibitisha kwamba Diamond mwenyewe hupenda mapozi hayo, kwa hiyo hupiga kwa ridhaa pamoja na bashasha ili aweze kuuza sura akiwa na shugamami wake.
ANACHOTAKA WEMA, DIAMOND HAPINGI
Uchunguzi unaonesha kuwa, Wema ndiye amekuwa kimbelembele kuelezea uhusiano wake na Diamond kupitia vyombo mbalimbali vya habari ndani ya Bongoland.

Bi mkubwa huyo, ameshakaririwa mara kadhaa kwenye redio, televisheni na magazeti akiweka wazi hisia zake kwa Diamond kuwa anampenda ‘dogo’ huyo na kwamba hapo ndiyo amefika.
Kutokana na tofauti ya majibu ya Diamond na Wema, ni wazi kuwa hata picha wanazopiga huwa ni matakwa ya ‘bi mkubwa, kwa hiyo ‘bwa mdogo’ hutekeleza bila kupinga wawapo chumbani.  
Wema alipozungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita alisema: “Mimi hizo picha hazinisumbui, nimeziweka ukurasa wangu wa Facebook. Sijali.”
MPAKA KITANDANI JAMANI!

Pamoja na picha nyingi kukosa maadili kwa sababu zipo ‘dipu’ kimahaba, baadhi zinaonesha kwamba Wema na Diamond wapo kitandani, wamejifunika shuka.
Kutokana na picha hizo, kuna mswali matano ya kujiuliza;

MOSI: Je, Wema na Diamond wanafanya majaribio ya kucheza filamu ya X?
PILI: Je, mshipa wa aibu umewatoka, kwa hiyo wanataka picha zao za chumbani zionwe mpaka na wazazi wao?

TATU: Siku hizi, watoto wadogo wanatembelea mitandaoni, je, wanataka walio chini ya miaka 18 (U-18) waone ili wawafundishe mchezo mbaya?
NNE: Kama ustaa ni kioo cha jamii, je, wao wanataka jamii ijifunze vitendo vya ngono kupitia kwao?
TANO: Je, wameshindwa kupiga picha zenye maadili kuwasilisha hisia zao mpaka ‘wakafotoa’ hizo za kuchakachuana?

KUTOKA RISASI JUMAMOSI
Picha chafu hazina tafsiri ya kukuza jina ili mtu awe maarufu, bali pia hazisaidii kuwasilisha hisia za kweli za mapenzi, kusema mtu akiziona atapata picha ya watu wanaopendana.


HABARI

No comments