Breaking News

ALBAMU YA “SHIKA HAPA ACHA HAPA” IPO JIKONI – H-BABA…!!


MSANII wa muziki bongo H-Baba,  atarajia kutoa albamu yake inayokwenda kwa jina la ‘Shika Hapa acha Hapa’, huku ikiwa na nyimbo 10.

Hayo yalisemwa na Meneja wa msanii huyo, ambapo alidai kuwa kabla ya kuachia albamu hiyo wataanza na video ya wimbo wao mpya ya ‘Sijalala’.

Hata hivyo alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwemo ndani ya albamu hiyo kuwa ni ‘Sijalala’, ‘Dogodogo’, ‘Shika Kichwa’, ‘Shika hapa acha hapa’, wimbo ambao umebeba jina albamu hiyo pamoja na nyingine kibao.

Meneja huyo alisema kuwa pamoja na kutoa kazi hizo pia kazi yake kubwa ni kumfanyia kazi msanii huyo kwani yenye ndiye mtu anayefanya promo ya H-baba.

“Mimi ni meneja wake hivyo hukusu ujio wa albamu hiyo najua utakuwa nzuri kwa sababu kwa sasa tupo katika maandalizi na baada ya kukamilika mashabiki wake watapata raha,” alisema.

No comments