Breaking News

QUICK RACKA AFIKIRIA KUACHIA ALBAMU MWAKA HUU…!!MSANII wa muziki bongo fleva, Quick Racka, amesema kuwa mwaka huu anafikilia kuachia albamu yake ya kwanza ili iweze kuwa zawadi kwa mashabiki wake.

Msanii huyo alitoa taarifa hizo, , alisema kuwa lengo lake ni kuachia ngoma moja moja, lakini kwa kufanya hivyo atakuwa ananyima radha mashabiki wake.

Rack alisema kuwa hata hivyo kwa sasa yupo katkka mchakato wa kurekodi nyimbo zake tatu ambazo hajazipa majina ambazo zitakuwa sokoni baada kukamilikia.

“Nafikilia kuachia albamu mwaka huu, lakini bado sijajua itakuwa na nyimbo ngapi kwa sababu lengo langu kubwa ni kutoa ngoma moja moja hivyo endapo nitajipaga vizuri basi albamu itakuwepo mwaka huu,” alisema.

No comments