Breaking News

CHERL COLE AMKOMOA COWELL.....


 
KITENDO cha Simon Cowell, kumtimua kazi Cheryl Cole, kinaonekana kuwa kilimuumiza sana mwanamuziki huyo mpaka kufikia hatua ya kulipa kisasi kwa namna ambayo haikutegemewa na wengi.
Simon Cowell mwanzilishi na mmiliki wa mashindano ya uimbaji ya X Factor Marekani na England, alimtimua kazi ya ujaji Cheryl Cole wiki tatu tu baada ya kufanya kazi katika shindano la Marekani.
Cole, ambaye aliwahi kuwa mke wa msakata kabumbu wa klabu ya Chelsea, Ashley Cole, ameamua kulipa kisasi kwa kufanya kazi na mpinzani mkubwa wa shindano la X Factor, The Voice.
Si tu amepata kazi katika shindano hilo, lakini mwanamuziki huyo huenda akazindua albamu yake katika kipindi hicho, kitu ambacho Cowell hajawahi kufanya katika shoo zake.

No comments